Mafanikio yoyote mazuri yanahitaji kuweka kazi kubwa sana kabla ya kuyapata na kuhakikisha kwamba kazi unaifanya kweli. Tatizo la kwa nini watu wengi sana hawapati kile ambacho wanakitaka ni kwamba wanagusa kila kitu na ila hawana kitu ambacho wanafanya.
Kuna watu kwa sababu tu za kizembe, hawataki hata kuambiwa ukweli. Na wanaogopa kusikia maneno ambayo yanawataka kufuata kanuni fulani ndogo ila zenye tijia kubwa sana. watu hawa wanajiita watu wenye fikra huru. Yaani LIBERAL THINKERS. Watu hawa wanatumia kigezo cha kuwa fikra huru kwamba wanaweza kufanya kitu chochote wanachotaka bila ya kuwa na nidhamu. Mwisho wa siku wanajikuta kwamba hawajaweza kufikia hatua kubwa sana kimafanikio, maana wanagusa hiki na kuacha na kwenda kugusa kitu kingine na kugusa na kingine bila ya nidhamu.
Ebu tuwashangae watu hawa kwa kuangalia mifano ya watu ambao binafsi najua wakijiita LIBERAL THINKERS na kuanza kufanya kitu chochote kwa wakati wanapotaka basi itakuwa hatari sana.
Fikiria rubani wa ndege ajjiite ni LIBERAL thinker, na aendeshe ndege kwa namna anavyotaka yeye bila kuwa na nidhamu……!!! Hivi hapa kitatokea nini? Basi kama sio kukupeleka wewe hapo nchi ambayo ulikuwa hutaki kwenda itakuwa ni kusababisha ajali…
Au dereva wa gari ambaye anajiita ni liberal naye akiendesha kwa namna ambayo anataka yeye itakuwaje?
Naomba tuishie hapo rafiki yangu, kitu kikubwa ni kwamba chagua kazi ambayo unaona utaweka juhudi na kazi katika kuifanya. Usihairishe na kukwepa majukumu yako eti kwa sababu wewe ni LIBERAL THINKER.
Usichelewe sehemu maksudi kila siku au mara kwa mara eti kwa sababu wewe ni LIBERAL THINKER.
Usikwepe majukumu yako eti kwa sababu wewe ni LIBERALL THINKER
Usiwadharau watu na kuwathamini baadhi ya watu eti kwa sababu wewe ni LIBERAL THINER
Tukutane kesho ashubuhi na mapema
Ndimi GGODIUS RWEYONGEZA.