TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-119 Tatizo ni hujajua kwamba unatafuta nini maishani mwako


Kijana mmoja kutoka katika mitaa ya scotland aliingia nchini Marekani na kuanza kufanya kazi za kawaida sana ambazo kila mtu angeweza kudharau. Kazi ambazo zilionenakana wazi kwamba ni kupoteza muda na zisingweza kumtoa kwa namna moja au nyingine. Aliishia kuwa miongoni mwa mabilionea wakubwa sana nchini Marekani.  Na kuna kipindi bilionea huyo huyo alikuwa na mamilionea zaidi ya 43 wakimfanyia kazi. kuna mtu alikuja kumuuliza Anderw Carnegie ni kwa jinsi alikuwa akihusiana na watu kiasi kwamba mamilionea wanakuja kwake kuja kumfanyia kazi. alikuwa na haya ya kusema. “kuishi na watu ni sawa na mtu ambaye anakuwa anatafuta dhahabu, ili kuweza kuipata dhahabu bora sharti kwanza utoe uchafu katika eneo ulilopo na kuuweka mpembeni, kabla ya wewe kupata kilo moja ya dhahabu utatakiwa kuhakikisha kwamba umeondoa tani na tani za uchafu ndipo unakuja kupata kilo moja, kwa kipindi chote cha kuondoa uchafu macho yako hayapaswi kuwa yanaangalia uchafu uko wapi, badala yake angalia dhdahabu”.
Katika dunia hii ili kuweza kuadika jina lako kwa ufasaha wa hali ya juuu sana na katika hali ambayo kila mtu ataifurahia basi kuna vitu ambavyo utatakiwa kuvifanya. Moja kati aya vitu ambavyo utatakiwa  kuvifanya ni hivi ambavyo tunajifunza kutoka kwa Andrew crnegie.

1.     Siku zote itafute dhahabu. Usitafute uchafu. Unapokuwa unaishi na watu mbali mbali hakikisha kwamba kila wakati unatafuta ubora katika watu badala ya kuangalia ubaya katika watu hao ambao unaishi nao. Kuna watu wao kuagalia ubaya katika watu ni sehemu ya maisha yao. Yaaani kila wakati wanaangalia ni kitu gani ambacho hakipo sahihi kwa watu wale ambao wanaoishi nao. Hili si jambo jema sana. wewe unapokuwa na watu kila mara jaribu kuangalia upande wa pili wa sarafu, yaani upande wenye mambo mazuri sana. hali kama hii hapa inawezekana.

2.     Watu wengi hawawezi kukuzia, kikwazo kikubwa sana hakiwezi kukurudisha nyuma, kelele nyingi sana haziwezi kukuzuia wewe hapo kuongea na kusikika. Isipokuwa wewe mwenyewe. Nimempenda Andrew Carnegie maana maisha aliyoanzia ni maisha ambayo mtu anaweza kusema kwamba ni maisha mabaya sana. kwa kipindi hiki na zama hizi hapa tulizopo tunaweza kusema kwamba Andrew Carnegie alikuwa mtumwa. Yaaniaalikuwa anafanya kazi ya kuajiriwa na kazi ambayo ilikuwa hailipi sana. lakini kilichokuja kutokea ni historia. Alilishia kuwa mmiliki wa viwanda vikubwa nchini marekani. Kumbe mahali ulipo sasa hivi hapana maana wala hapawezi kutwambia kwamba kesho yako itakuwaje. Badala yake kile ambacho unafikiria katika akili yako ndicho kitatuambia ni wapi ambapo unapenda kwenda na ni wapi unataka kufika. Kumbe hii ndio kusema kwamba naweza kuandika jina lako kwa ufasaha wa hali ya juu sana bila kujali kwamba kwa sasa uko katika mazingira gani. Bado nafasi ya kuandika jina lako likasomeka vizuri sana ipo na watu watakaa na kuanza kujiiuliza hivi hili ni jina lile ambalo hapo awali lilikuwa limeandikwa vibaya na halionekeni kabisaaa! Muda wako wa kuandika jina lako na kuhakikisha kwamba umeleta utofauti hapa dunini ni sasa hivi. Haijalishi umri wako ni miaka mingapi. Kitu kikubwa sana ambacho unaweza kufanya ni kutafuta sababu ya kwa nini wewe hapo unapaswa kuanza, sababu moja tu inakutosha wewe kuweza kuanza na kufanya makubwa sana katika dunia hii ambayo watu tunaishi.


3.     Haijalishi wewe hapo unahitaji kuandika jina lako kwa naman gani. Ila kitu kikubwa sana ambacho unapaswa kuhakikisha kwamba umekizingatia ni kwamba  unapaswa kujenga msingi mkubwa sana. ghorofa kubwa ndefu huwa haijengwi kwa kuanza na ghorofa ya mwisho bali huwa inajengwa kwa kuanza na msingi mkubwa sana ambao unaaenda chini kabisa. Ukitaka kujua umbali wa ghorofa sharti uangalie umbali wa msingi ambao umejegwa. Kadri msingi unavyokuwa umeelekea chini kabisa ndivyo na ghorofa itakavyoinuka juu kabisa. Inawezekana wewe upo katika kipindi cha kujenga msingi wako. Kipindi ambacho unapaswa kuchimba kuelekea chini kabla ya kuanza kupanda juu. Kipindi hiki kinaitwa majina mengi sana. wengine wanakiita kipindi cha giza kuuelekea mwanga, huku wengine wakisema ni kipindi cha ijumaa kuu kuelekea pasaka. Haijalishi utakiitaje ila ukweli ni kwamba lazima kitaisha tu na kipindi cha mwanga wa kutosha au pasaka kitafika. Na hapo utakuwa na wakati mzuri sana wa kufurahia maisha na kufanya vitu vingine zaidi. Kumbuka kwamba urefu wa msingi ndio utakaokwambia aina ya nyumba ambayo utaijenga. Na muda mwingine unaweza kukuta kwamba msingi ambao umeujenga kwa chini una uzito mkubwa sana kuliko hata sehemu nyingine ya jengo kwenda kwa juu.  Kumbuka kwamba msingi huu ni sehemu ya jengo. Ujenge vizuri sana.

HAKIKISHA KWAMBA UNAJIFUNZA KUANDIKA JINA LAKO VIZURI SANA. NA JINA LAKO LINAANDIKWA HIVI.


Umekuwa nami,
GOIUS RWEYONGEZA
($onga mbele)
Tuwasiliane,
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

Sasa unaweza kujipatia vitabu  vyangu vyote kwa bei  yz zawadi. Hahahah! Hii inaitwa ya kwako tu! Unaweza kupata vitabu hivi hapa kwa shilingi 14,000/- badala ya 20.000/- cha kufanya,  lipia kupitia nambari  0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo nitumie ujumbe wa kuniambia ni njia gani ambayo ungependa mimi hapa nikutumie vitabu. Vitabu vunatumwa kwa njia ya email wasapu au telegram. Karibu sana.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X