TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-121 Tatizo hujanoa shoka lako


Kuna mashoka tunayatumia kila siku katika kazi zetu mbali mbali. mashoka haya huwa yanapungua makali kadri yanavyokuwa yanatumika zaidi na hivyo kufikia hatua ambapo makali hupotea kabisa. Imekuwa hivi, kwa siku nyingi sana, na itaendelea kwua hivi. Hii ndio kusema kwamba lazima kila utakapotumia shoka leo lipungue makali na hivyo ukija kulitumia shoka hilo kesho basi litakuwa limepungua makali yake kulingana na jana yake. Lakini katika hali ya kawaida shoka ulilotumia jana halipaswi kuwa si bora kama la leo. Hii ndio kusema kwamba shoka unaloenda kulitumia ndani ya siku hii ya leo, linapaswa kuwa na makali zaidi. Kabla sijakwambia jinsi ambavyo unaweza kunoa shoka lako likawa lenye makalil kila mara naomba tujifunze kutoka kwa watu hawa wawili.
Katika kampuni ya songa mbele iliyopo nchini Tanzania kuna vijana wawili, kijana mmoja anaitwa TOM na mwingine anaitwa JOH. Joh kaajiriwa kwenye kampuni hiyo zaidi ya miaka 7 iliyopita, wakati Tom kaajiriwa na huu ni mwaka wa pili. Watu hawa wapo kwenye kitengo kimoja. Japo Joh alimtangulia mwenzake kazini, lakini kwa sasa Tom amependishwa cheo mara mbili zaidi ya rafiki yake.
Siku moja Joh alimfuata mkurugenzi na kumuuliza, kulikoni, mbona mimi sipandshwi cheo?
Mkurugenzi alikuwa na haya ya kusema, mimi sijui kwa nini hujapandishwa ila ukweli ni kwamba Tom anafanya kazi zaidi yako,, meneja aliendelea kusema kwamba hivyo unapaswa na wewe kwenda na kuweka juhudi na kuhakikisha kwamba unafanya kazi zaidi ya rafiki yako. alienda kuweka juhudi kusudi apandishwe cheo. Lakini mabadiliko hayakuonekana. Na kwa kuwa kazi yao ilikuwa ni kukata miti ya mbao. Joh aliendelea na kasi yake ya kukkuta miti mitano kwa siku wakati mwenzake Tom akikata mara mbilil zaidi yake.
Baaada ya siku chache sana, Joh alirudi kwa meneja na malalamishi yake ya kwamba ameashindwa kitu cha kufanya ili aweze kupandishwa cheo. Bosi yake alumwambia, sijui ila nenda umuulize Tom bila shaka ana mengi ya kukueleza. Basi Joh alipiga safari yake na kwenda kwa Tom na kumuuliza “inakuwaje wewe unakata miti zaidi ya mimi kila siku’?
Tom alijibu kwa kusema yafuatayo, “kila baada ya kuukata mti mmoja huwa nakaa chini na kunoa shoka langu”
Kumbe kunoa shoka ni muhimu, muhimu, muhimus sana.
Je, shoka lako ni lipi?
Bila shaka mpka hapo utakuwa ukijiulilza shoka langu linaaweza kuwa kitu gani? Hapa ninayo mashoka matano ambayo kwa haraka unahitaji kuyanoa. Hakikisha kwamba unafanya hivyo kuanzia sasa. Mahusiano, fedha, elimu, afya na kazi. haya ndio maeneo muhimu unayoapaswa kuboreha kuanzia sasa, na hivi ndvyo unaweza kuyaboresha.
#1. MALENGO
Unapaswa kuhakikisha kwamba malengo yako unayapitia kila siku na kuongeza maarifa mapya ambayo unayapata kila siku. Kamwe usikubali malengo yako ipite siku hujafanya hatua yoyote ile ambayo inakusogeza na kukuwezesha kuweza kuyafikia. Hakikisha pia unayaandika kila siku na kutembea na KARATASI YA DHAHABU (rejea KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI ukurasa wa 35-37 na ukurasa wa 86). Malengo pia yaweke katika matendo kila kunapokucha. Kwa hakika kama utafanya hivi, basi jua kwamba utakuwa umenoa shoka lako kwa uhakika
#2. KUHUDHURIA SEMNINA
Unapaswa kuwa unahudhuria semiina zisizopungua tatu kila mwaka. Ndani ya semina hizi utanolewa na kuongezewa nguvu mpya, hali ambao itakufanya upate shoka lenye makali sana kuliko shoka jingine lile.
#3. SOMA VITABU
Kusoma vitabu ni njia nyingine ya kuongeza maarifa na kunoa shoka lako. Hakikisha kwamba kila siku unasoma kitabu walau kwa nusu saa. Hata kama umebanwa kiasi gani, ninaamini dakika thelathini unaweza kuzipata kla siku
#4. Kaa kimya
Moja kati ya vitu ambvyo ni vigumu sana kuvipata katika dunia hii ni utulivu kutoka kwa watu. Kila sehemu kuna kelele nyingi sana. na asilimia kubwa ya kelele ni za malalamishi. Watu wanalalamika kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi, wanalalamika mvua imenyesha, watu wanalalamika mvua haijanyesha, yaani mimi sielewi malalamishi haswa ya watu ni yapi. Maana kwa jambo jema wanalalamika, jambo linaloenda kinyume na matarajio wanalalamika sasa hapo ndipo kabisaaa sijui shida ni nini! Ila wewe cha kufanya, kaa kimya na fanya kazi tena kwa bidii ya hali ya juu sana.
#5. Anza kuishi
Ndege mmoja aliye mkonni ni bora kuliko ndege kumi walio mbali. vivyo hivyo kwentu kwa maisha ya kila siku, sekunde moja ya sasa hivi tuliyonayo ni bora zaidi kuliko mamilioni ya sekunde ya kesho. Hivyo itumie vyema sana sekunde ya leo. Ishi leo kwa kufanya kile kilichobora sana ndani ya siku hii ya leo. Ishi leo, fanya leo.
Unaweza sasa kujipatia vitabu vyangu kwa bei ya zawadi ambao ni tsh.14,000 badala ya 20,000. Bei hii ni ya muda na itadumu ka kipindi kidgo mpaka tarehe 10 mwezi huu.
Vitabu hivi ni TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA ambacho kama utakichukua peke yake bei yake ni 6,000 badala ya 10,000.
KUTOKA ASIFURI MPAKA KILELENI ambacho bei yake ni 8,000 badala ya elfu kumi. Lipia sasa kupitia namabari ya simu ifuatavyo,
0755848391 jina GODIUS RWEYOLNGEZA.

karibu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X