TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-122 Tatizo hujajua maana ya ujana


TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-121
Tatizo hujajua maana ya ujana
Vyanzo mbali mbali vya taarifa na maarifa vimetoa maana kadha awa kadha za ujana. Maana hizi zimetolewa kwa misngi na mitazamo flani flani. Kwa mfano kuna watu wanaoamini kwamba uana ni maji ya moto. Bila shaka hawa wanalenga kusema kwamba ujana ni kitu cha muda mfupi na hivyo unapaswa kuutumia kadri uwezavyo.
Wengine wanasema kwamba ujana kipindi kati miaka 15 mpaka 35. Hawa wametoa maana kwa kuangalia umri wa mtu
Wengine wanasema kwamba ujana ni kipindi cha mpito.
Kurasa za kamusi ya Kiswahili sanifu zimetoa maana ya ujana kama ifuatavyo, “umri kati ya utoto na utu wa makamo”.
Binafsi nimezipenda maana zote hapo juu ingawa sijaona maana ya  kweli ya kijana. Haruwezi kuishia tu kusema kwamba ujana ni maji ya moto. Then what?
Au hatuwezi  kusema tu kwamba unaja ni umri kati utoto na utu uzima, kwa hiyo nini sasa?
Binafsi niingependa maana ya ujana ikae hivi, UJANA NI KIPINDI CHA KUJIFUNZA, KUFANYA MAJARIBIO NA KUKUA.
Ukiangalia maana hiyo hapo juu utakuta kwamba ndani yake kuna vitu vikuu vitatu,
1.     KUJIFUNZA
Kipindi cha ujana ni kipindi ambacho unapaswa kuhakisha kwamba unajifunza vitu vingi sana. ni kipindi ambacho hupaswi kuridhika na maarifa yale uliyonayo. Bali ni kipindi ambacho kila mara unapaswa kuhakikisha kwamba unaongeza maarifa kwa kuyatafuta katika vyanzo mbali mbali. na maarifa haya yapo, kinachosubiriwa ni utayari wako na kuhakikisha kwamba unayatumia maarifa haya.
2.     KUFANYA
Ndani ya kipidi hiki unapaswa kuhakiisha kwamba unafanya vitu mbali mbali. mwanzoni nimesema kwamba haupaswi kuridhika na maarifa uliyonayo. Vivyo hivyo hupaswi kuridhika na vitu vichache ambavyo umefanya katika ujana wako. Kila siku ya ujana wako itumie kuhakikissha kwamba unafanya kitu kipya ambacho jana yake hukufanya. Utumie ujana, utumie haswa,
Kama wewe ndani ya kipindi hiki unafanya biashara, basi usiridhike na biashara moja katika eneo moja. Hakikisha kila siku ya ujana wako unaitumia kukuza mtandao wa biashara  yako. hakikisha biashara yako inamfikia hata mtu aliye kiijini kule mbali sana kutoka hapo ulipo. Iga kwa watu wa coca cola. Coca cola kwa sasa imesambaa takribani ulimwenguni kote. Kuanzia mashariki, magharibi, kasikazini na hata kusini. Na wewe pia fanya hivyo. 
3.     KUKUA
Watu walio wengi wamezoea kwamba kukua ni kuongezeka kwa kimo. Hahahah! Kukua hakumaanishi kuongezeka kwa kimo tu! Kukua kuna vitu vingine vya ziada, ikiwemo  kuongezeka kwa busara, amani ya akili, maarifa ya kutosha na kujiongoza mwenyewe. Na kuna njia nyingi sana ambazo unaaweza kuzitumia ili kukua. Njia mojawapo ni kujifunza. Kufanya pia kunakufanya ukue. Na kukua ni kwa kila siku wala sio kwa siku moja tu! Kukua ni mchakato endelevu na wa kila siku. Kadri unavyofanya vitu vipya ndivyo unavyokua, na kadri unavyokua ndivyo unavyokuwa unajifunza zaidi. Ukiona umepitisha siku bila kukua basi jua kwamba unajichimbia kaburi lako wewe mwenyewe. Hakikisha kwamba leo umekua. Na kipimo kizuri cha kukua sio kile cha kuongezeka kwa kimo. Kipimo kizuri ni kile cha wewe kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana.  je, kitu gani utafanya leo kitakachoonesha kwamba umekua!?
Kumbuka vitu hivi vitatu vinaenda kwa kufuatana kama ambavyo nimeelezea hapo juu. Kujifunza kutasababusha ufanye, na kufanya kutakuleta kwenye kukua. Lakini ukishakua utapenda kuendelea kuifunza zaidi. Hivyo kinachokuja kutengenezwa kutoka hapo juu ni mduara, hii ni kutokana na kwamba kimoja husababisha kingine, na kingine kusababisha kingine kama ambavyo imeoneshwa hapa chini. Kumbuka kujifunza hakujachukua nafasi mpaka pale utakapokuwa umekuweka kwenye matendo (kufanya). Na kufanya siku zote kunaambatana na kujifunza kitu kipya, Maana siku zote hujui kitu mpaka pale utakapokuwa umekifanya
  
KUJIFUNZA
 


  KUKUA                                         KUFANYA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X