TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-126 tatizo hauna kiu ya kutoshaKuna kijana mmoja alimwendea Socrates ili kumuuliza siri ya mafanikio katika maisha. Socrates alimwabia kijana huyo wakutane siku inayofuata kwenye mto uliokuwa karibu yao. Kesho mapema socretes na kijana walikutana kwenye mto. Socretes alimwomba kijana watembee kwa pamoja kwenye mto ule. Walianza kutembea kwa pamoja huku maji yakizidi kuongezeka kina. Maji yalianzia kwenye miguu hatimaye yakawa yamewafikia kwenye shingo. Ni katika hatua hii ambapo Socrates alilamua kumzamisha kijana majini bila huruma na kwa kumshutukiza. Kijana alitapatapa ili aweze kutoka ndani ya maji lakini Socrates alikuwa amemshikilia kwa nguvu sana kiasi kwamba kijana hakuweza hata kutoa kichwa. Huku kijana akiwa katika hali mbaya,Socrates aliamua kumwachia kijana ili atoke ndani ya maji. Mara tu baada ya kijana kutoka ndani ya maji kitu cha kwanza alivuta pumzi kwa nguvu. Socrates alimwambia kijana ni kitu gani ambacho ulikuwa unakihitaji sana ulipokuwa ndani ya maji. Kijana alijibu “hewa”. Basi Socrates alimwabia kijana, kiu uliyokuwa nayo ili kuweza kupata hewa ni hiyo hiyo unapaswa kuwa nayo katika kuhakikisha kwamba unatafuta na kuelekea mafanikio. Hakuna siri nyingine.

Rafiki yangu somo la leo li wazi kabisa. Naomba na wewe ukaweke juhudi na nguvu katika kazi kwa kutumia ujumbe huu huu ambao Socrates alimpa kijana. Tukutane kileleni.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
Jipatie nakala ya vitabu vyangu vyote kwa bei ya zawadi ya shilingi 14,000 tu. Bei hii ya zawadi mwisho wake ni tarehe 10. february mwaka huu.  Baada ya hapo vitabu hivi vitaanza kupatikana kwa bei yake ya kawaida abayo ni tsh. 20,000. Hakikisha unaichangamkia zawadi hii rafiki yangu kwa kulipa kiasi hicho kidooogo kwenda nabari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo nitumie ujumbe wa kunijulisha juu ya njia ambayo napaswa kuitumia[ss1]  ili kukutumia kitabu hicho. Ambayo inaweza kuwa ni wasapu, telegram au email Karibu sana,
Bei ya kitabu kioja ni TATIZO SI RASILIMALI ZILIOZPOTEA- sh. 6,000/-
KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI tsh 8,000
Vitabu vyote ni soft copy na vinatumwa kwa email, wasp au telegram.

Ulikuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X