TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-128 Tatizo hujajua umuhimu wa kusoma vitabuNi katika vitabu pekee unaweza kuongea na watu maarufu, unaaweza kuongea na viongozi wakubwa, unaweza kuongea na wafanya biashara, unaweza kuongea na wajasiliamali, unaweza pia kuongea na wajasiliapesa….Aliandika mtu mmoja.
Kama ambavyo tumeona kwenye kidokezo hicho hapo. Vitabu vinakufanya wewe uweze kuungana na kuongea na watu wengi sana. unaongea na watu walio ndani nchi pamoja na watu walio nje ya nchi. Vitabu vnakufanya uongee na watu hawa kwa sababu muda mwingine watu hawa wanakuwa mbali na wewe, ila ukitaka kujua juu ya mawazo yao basi unapaswa kutafuta vitabu na kuhakikisha kwamba umevisoma. Kwa kufanya hivyo utakuwa umejihakikishia ushindi mkubwa sana.
Je, leo unaenda kuongea na nani? Chagua kitabu sasa cha mtu ambaye utaongea naye.
NDIMI,
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X