Tukiufahamu uwezo wetu tutakuwa kama ndege, tutaruka bila hofu. Tukiufahamu uwezo wetu tutakuwa kama mbegu, yaani tutaota bila kujizuia na kuzalisha msitu. Tukiufahamu uwezo wetu, tutaamua kufanya na tutafanya bila uoga.
Kumbe ndio maana Eckharat Tolle anatuambia kwamba “hauwi mzuri kwa kujaribu kuwa mzuri, lakini kwa kutafuta uzuri ambao tayari umo ndani yako”. kumbe tayari wewe hapo unao uzuri ndani yako, usiutafute kwa nje, wala usijaribu kuwa mzuri. Usijihofie wewe ni zaidi ya ulvyo sasa hivi.
#1. Swali la muhimu la kujiuliza hapa ni je, ningejua kwamba sitashindwa kitu gani kimoja ambacho nitafanya? Orodhesha vitu ambavyo unajua kwamba utafanya kama usingeshindwa baada ya hapo chukua hatua madhubuti, usisubiri mazingira yakae vizuri, anza kufanya kidogo kidogo. Anzia hapo ulipo. Mtu pekee wa kubadilisha mazingira ni wewe. Na mtu mkubwa wa kufanya mabadiliko ni wewe.
#2. Chukua hatua ndogo ndogo kama mtotot mdogo. Jiweke katika hali ya kujifunza kila siku. Huhitaji kuwa unajua kila kitu ili uanze. Unaachohitaji kufahamu ni mtu gani wa kuita! Weka juhudi zaidi na fanya zaidi.
#3. Jipongeze kwa kila hatua ambayo unachukua. Hii haijalishi umepiga hatua kidogo au kubwa sana. bado unapaswa kujipongeza, mafanikio makubwa huwa hayaji kwa siku moja. Bali huwa ni mwendelezo wa kile ambacho unakuwa unakifanya kila siku
Asante sana imani yangu kwamba utachukua hatua madhubuti sasa na kuzidi kuisonga mbele.
Jipatie vitabu vyangu viwili kwa shilingi 17,000 tu! Yaani unapata KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kwa shilingi 9,000 tu! Na TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA kwa sh. 7,000 tu. Cha kufanya sasa ni kulipia pesa kwenda nambari 0755848391 jina la MPESA ni GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo nitumie ujumbe mfupi wenye email yako ili niweze kukutmia vitabu hivyo. Karibuni sana, kitabu kimoja kimoja pia kinapatikana kwa bei iliyotajwa hapo juu.