TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-136 Tatizo hujajua umuhimu wa soma kitabu


Kitabu kimoja kina uwezo wa kubadlisha maisha ya mtu na kuyafanya kuwa ya tofati. Ila watu kidogo sana wanaweka juhudi kuhakikisha kwamba wanasoma na kuyatumia maarifa haya yaliyomo kwenye vitabu. Ukiongea na watu walio wengi utawasikia wakisema kwamba wao kusoma vitabu sio hobby yao. Wengine wanajisifia kwamba wao ni magwiji na hivyo hawahitaji kupata maarifa ya kwenye vitabu maana maarifa wamezaliwa nayo kwa asili. Na hapo ndipo huwa wanaendelea kusema kwamba wale ambao huwa wanasoma vitabu ni vilaza ndio maana husoma vitabu ili waweze kuondoa ukilaza ulio ndani yao. Wengine huenda mbali kwa kusema kwamba kusoma vitabu ni kuishi maisha ya watu wengine ndio maana wao hawasomi vitabu.
“ukitaka kujua utamu wa ngoma sharti uingie ucheze”, ni maneno ya wahenga. hivyo hivyo kwa watu wengine ambao wao wanasema kwamba hawawezi kusoma vitabu, au ambao wana majibu kama ambayo yametolewa hapo juu, basi jibu la haraka haraka ambalo unaweza kumwabia mtu ni kwamba ngoma hainogi kwa kuwaangalia wachezaji wakicheza, bali hunoga kwa mtu mwenyewe kuingia uwanjani na kuhakikisha kwamba amecheza. Kama ulikuwa bado hujaanza kusoma kitabu chukua kimoja leo na ukisome na tuone kama kweli malalamishi yako juu ya vitabu ni kweli au la!
Huwezi kuhukumu kitabu kwa ganda  lake ni msemo mwingine wa waswahili. Hapa huwa wanataka kusema kwamba  huwezi kutoa hoja ya kukashifu kitu au kukisifia wakati kitu chenyewe hujakiona kabisa. Jambo hili si jema hata kidogo. Na wewe pia hupaswi kuhukumu vitabu kabla ya wewe kuanza kusoma hata kimoja. Cha kufanya wewe soma kimoja tu baada ya hapo utaniambia ni kweli maneno ya watu juu ya vitabu ni sahihi au!
Jilazimishe hata kama hujisikii kusoma kitabu, ila kwa kuwa ni kimoja basi tu wewe soma.
Swali je nianze na kitabu gani, kiukweli vipo vitabu vingi sana, unaweza kuchagua chochote kile ambacho utaona kwamba wewe kinakufaa sana, kulingana na kile ambacho unapendelea maishani,
Kama bado hutakuwa hujapata basi chukua kitabu kimoja kati ya hivi, KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI pamoja na TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA. Soma kimojawapo na baada ya hapo utanipa jibu.
Vitabu hivi vyote vinapatikana kwangu katika mfumo wa nakala tete (soft copy). Na vinauzwa kwa shilingi 10,000 kila kitabu.
FAIDA YA KUNUNUA KITABU HIKI LEO, kwa yeyote atayenunua kitabu kimojawapo ndani ya wiki hii, yaani kuanzia tarehe  23 februari mpaka tarehe 1 machi atapata kitabu kingine kimoja buree kama zawadi. Na kitabu hiki si kingine bali ni kitabu cha NYUMA YA USHINDI, KUNA KUSHINDWA, KUSHINDWA, KUSHINDWA….
Zawadi hii itatolewa kwa watu wote watakaonunua kitabu kimojawapo kati ya vitabu viwili hapo juu. Na zawadi hii itatolewa rasmi jumapili ya tarehe 4 machi.
SWALI, je kama tayari nimenunua na kusoma vitabu vyote nitaipataje zawadi hii?
Vizuri, kama tayari umesoma kitabu kimoja wapo kati ya hivyo hapo ni vyema sana. zawadi ya kitabu hiki cha NYUMA YA USHINDI na vingine zaidi vitaendelea kukujia kila mwezi ndani ya kundi la HAZINA YETU TANZANIA. Yaani mwezi wa nne utakuwa na kitabu, wa tano kitabu kingine, wa sita kitabu kingine tena buree kabisa. Na tena vitabu vya Kiswahili. Cha kufanya ni kuhakikisha kwamba unakuwa mwanachama wa HAZINA YETU TANZANIA. Ili kuwa mwanahazina yetu Tanzania unaalipia ada ya kuwa mwanachama wa kikundi cha HAZINA YETU TANZANIA ambayo ni 20,000 kwa mwaka.
Kwa wanachama wote wa hazina yetu vitabu hivi ni bure kabisa na hakuna kitu kingine ambacho unaweza kufanya zaidi isipokuwa kuendelea kuwa kwenye kundi, baasi.
Sasa nalipaje? Pesa yote utatuma kwenda mpesa nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA, baada ya hapo nitumie neno lenye jina la kitabu na email yako. nitakutumia kitabu ndani ya muda kidogo baada ya wewe kutuma pesa. Kama utakuwa umelipa kwa ajili ya HAZINA YETU TANZANIA, basi utanitumia ujumbe wenye neno HAZINA, ili nikuunganishe.
Tukutane kileleni
#NYUMA_YA _USHINDI
Ndimi,
GODIUS RWEYONGEZA
($onga mbele)

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X