TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA _125 Tatizo unaomba msaada pasipostahili


Kuna nyakati wakati tuna kuza na kuendeleza vipaji vyetu vilivyo  ndani yetu huwa tunaona kwamba basi hapa ni bora kabisa kuhakikisha kwamba tunatafuta msaada kwa watu  ili waweze kutusaidia. Tunatafuta watu wa kutuwezesha kupiga hatua. Na pengine mtua anatafuta wazazi wake akijua haswa kwamba wao ndio watakaoshughulika na mawazo yake na kuhakikisha kwamba kile ambacho yeye anafikiria basi wazazi wake ndio wanafanya kazi kubwa sana. kama anafikiria juu ya uwekezaji basi anafikiri kwamba wazazi wake ndio wanapaswa kuhakikisha kwamba wanawekeza kwa niaba yake. Kama ni kuinuka na kuwa na maisha bora basi muda wote ana kuwa anawategemea wazazi wake wawe wa kwanza kufanya hivyo.
Ukweli ni kwamba kadri watu wanavyokuwa wanakusaidia wewe hapo ndivyo wanavyokuwa wanakuharibu wewe hapo na kukupunguzia uwezo wako wa kujiimarisha.
Kuna mwalimu mmoja alikuwa anafundusha somo la sayansi kwa wanafunzi wake. Mwalimu yule aliwaambia wanafunzi wake kwamba kiwavi huwa anahangaika kutoka kwenye maganda yake. Baada ya mahangaiko mengi kiwavi huyo atatoka na kuwa kipepeo kamili. Mwalimu huyo aliondoka darasani na kuwaacha wanafunzi wa somo la sayansi wakiendelea kumwangalia yule kiwavi. Ilifikia hatua mahangaiko yakawa mengi sana kiasi kwamba mwanafunzi mmoja akamhurumia kiwavi na kutoa baadhi ya maganda, ili kiwavi aweze kutoka vizuri. Mwanafunzi akawa amesaidia kiwavi kutoka lakini baada ya muda kiwavi alifariki. Mwalimu alirejea tena darasani kuendelea na kipindi. Alikuta kiwavi amefariki mezani. Ndipo wanafunzi walianza kuelezea kilichotokea. Mwalimu alikuwa na haya hapa ya kusema. Katika hali ya kawaida, kiwavi hahitaji msaada ili kutoka kwenye maganda yake na kuwa kipepeo. Ukimsaidia ndio unakua unamharibu kabisa. Mahangaiko yale ya kujitoa kwenye ganda ndio yanayomwimarisha.
Hali hii ndio inayotoke katika maisha. Wazazi haawapaswi kuwa kikwazo kwa watoto wao kuweza kukuza vipaji na ubunfu ambao wanao ndani yao. Bali wazazi wawe watu wa kuwaongoza watoto wao kuhakikisha kwamba wanaendeleza vipaji na ubunfu walio nao. Kuna nyakati wazazi wanaweza kuwa wanafikiri kwamba kwa kuwaonea huruma watoto wao ndio wanawasaidia kumbe wanawaharibu kabisa maana wanatoa ganda la nje ambalo ni muhimu sana mtoto alipitie ili kuweza kukua zaidi. Siku zote hujakua  kama hujapitia katika changamoto. Kwa hiyo hakikisha kwamba kila wakati unajifunza kutokana na changamotoa ambazo unakutana nazo kila wakati kila sehemu.
BAHARI SHWALI HUWA HAITOI WANAMAJI  MAKINI

Maisha bila matatizo sio maisha. Matatizo ndio hutufanya tukue na kuzidi kusonga mbele. Nyakati mbaya ndizo zimeweza kuwaimaisha na kuwatoa wanamaji stadi. Kitu kikubwa katika kuendeleza ubunifu wako sio kuacha. Bali ni kuhakikisha kwamba unaendelea na kupambana mpaka pale utakapokuwa umeweza kufikia mwisho wa kilele ambacho unakifikiri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X