TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA Tatizo hujajua nguvu yako uliyonayo


Kila mtu kazaliwa akiwa na nguvu kubwa sana ambayo Imo ndani yake. Kama nguvu hii itatumiwa vyema sana itaweza kumsaidia mtu kuweza kupiga hatua. Iko hivi kila kitu tunachofanya hapa duniani ni matokeo ya nguvu ambayo imo ndani yetu. kila wazo tunalotoa ni nguvu, kila mtu tunayeongea naye tunatumia nguvu.
Ukiwaza hasi unatoa nguvu hasi, na ukiwaza chanya unakuwa unatoa nguvu chanya. Kile ambacho unakuwa unakiwaza mara kwa mara ndicho kinakuja kukufanya wewe kuwa jinsi ulivyo. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kukufanya kuwa jinsi ulivyo tofauti na wewe hapo.
Kwa hiyo unaweza kuamua kuwekeza na kuamua kuzitumia vyema sana nguvu zako kwa ajili ya vitu ambavyo ni vya muhimu sana katika maisha yako. na vitu hivi  nivile ambavyo vinakupa thamani. Kumbuka kwamba ukiwekeza muda wako na nguvu yako katika kufanya vitu ammbavyo havina maana mwisho wa siku utajikuta kwamba unanachoka wakati ukiwa hujafanya kazi za maana kubwa sana. jenga utaratibu wa kuwekeza nguvu zako kwa kufanya vitu vyenye maana kubwa sana  maishani mwako.
Sio lazima ufanye kila kitu. Ila chagua vichache ambavyo utawekeza nguvu yako kuhakikisha kwamba unapata matokeo makubwa sana maishani mwako. Itumie nguvu ya wewe.
Baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kukupotezea nguvu yako ni kama ifuatavyo
Mabishano
Mawazo hasi
Kuangalia televisheni
Kusikiliza taarifa ya habari
Kufikiria yo hata havilujengi
Kufikiria ambavyo hata havitakuja kutokea
Hivi ni  vitu ambavyo unapaswa kuhakikisha kwamba unaepukana navyo.  Kila mara unapotoa nguvu hasi mwili wako unakuwa unatoa homoni mwilini ya stress na kila unapoa nguvu chanya mwili wako unatoa homoni ya furaha. Acha kujiangamiza kwa kutoa homoni hii ya stress. Anza kufanya vitu chanya na anza kushi katika namna ya uchanya. Kwa nini ujinyime furaha wakati unaweza kuwa mwenye furaha muda wote.
Ulikuwa nam,
GODIUS RWEYONGEZA

($onga mbele)


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X