Viashiria Vitano (05) Vitakavyokufanya Uendelee Kuwa Maskini Maisha Yako Yote


Habari ya siku hii ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa  makala kutoka blogu yako pendwa ya songa mbele. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako na unaenda kuweka juhudi kuhakikisha kwamba unaenda kufanya mambo makkubwa sana ndani ya siku hii ya leo. Karibu sana tuweze kujifunza kwa pamoja jambo ambalo litatupa nguvu ya kusonga mbele ndani ya siku hii ya leo.
Miongoni mwa vitu ambavyo kila binadamu angependa kupata maishani mwake ni mafanikio ya kipesa. Kila mtu angependa kupiga hatua na kuhakikisha kwamba anatoka kwenye lindi la umasikinikwenda hatu ya ziada yaani kwenye utajiri. Hakuna mtu ambaye anafurahia na kupenda na hali hiyo hiyo kila siku. Japo watu wengi hawapendi hali zao walizonazo, ni wachache sana ambao wanachukua hatua kuhakikisha kwamba wanaifanyia kazi hali ambayo wanayo kwa sasa. Yaani watu ambao wanachangamka kuhakikisha kwamba wanaibadili hali ya sasa ili iweze kuwa hali yenye matunda kwa siku za mbeleni ni wachache sana. sasa hapa nimekupa vitu vitano ambavyo vitakufanya uendelee kuwa masinin maiha yako yote kama hutavitilia maanani na kuhakikisha kwamba unachukua hatua kuvibadilisha. Na kumbuka kwamba hakuna mtu yeyote yule ambaye anaweza kuleta mabadiliko makubaw sana maishani kama sio wewe hapo kuchukua hatua na kuweza kusonga mbele. Sasa vitu hivyo hapo ni kama ifuatavyo

#1. UKOSEFU WA NIDHAMU YA PESA
Pesa ina nidhamu yake ambayo unapasaw kuwa hnayo ili uweze kuzidi kusonga mbele na kupiga hatua kubwa sana maishani mwako,  si kila pesa ambayo unaipokea lazima uitumie papo hapo. Lazima siku zote uwe na nidhamu ya hali ya juu sana katika kufanya kitu ambacho umepanga kufanya. Hauwezi kupiga hatua katika masula ya kipesa kama utaendendelea kufanya vitu vile ambavyo ulikuwa unafanya mpaka ukafika hapo ulipo. Kwa hiyo ili wewe hapo uweze kupiga hatua na kuhakikisha kwamba unaweza kusonga mbele, huna budi kuhakikisha kwamba unachukua hatua za tofauti ili kuweza kusonga mbele zaidi. Hivyo nidhamu ya pesa ni muhimu sana kwako kuhakikisha kwamba unakuwa nayo. Hakikisha kwamba hautumiii kiasi kikubwa zaidi ya kile ambachounaingiza. Hakikisha pia haujengi utaratibu wa kujikopa mara kwa mara kutoka kwa watu wengine. Weka akiba kwa ajili ya matumizi yako ya siku za mbeleni. Yaani linapokuja suala zima la pesa basi hakikisha kwamba pesa yako unaifanyia kazi kwa mambo ambayo ni ya muhimu sana.

#2. UKOSEFU WA NIDHAMU YA MUDA
Muda ni suala la muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Kila mtu kapewa masaa yale yale kila siku. Hakuna mwenye zaidi wala mwenye kidogo. Yaani watu wote wana masaa sawa sawia. Lakini matumizi ya muda miongoni mwa watu ndio hutofautiana. Wapo ambao hutumia muda wao vizuri na kuhakikisha kwamba wanaweza kupiga hatua za kimaisha.Hatua ambazo huwa zinawatoa sifuri na kuhakikisha kwamba zinaweza kuwafikisha kileleni. Lakini wapo  ambao ndani ya muda ule ule ambao wachache wanautumia kufanikiwa wao wanautumia kujiangamiza. Hawautumii vizuri wala hawana nidhamu na muda wao. Kwa hakika ni vigumu sana kufanikiwa kama utaendelea kufanya vitu kwa namna ile ile kila siku bila kuhakikisha kwamba unafanya mabadiliko. Muda wako ni rasilimali yako nambari tatu baada ya akili na nguvu kiinachofuata ni muda. Je, wewe unautumia muda wako kufanya kazi gani? Fanya vitu ambavyo ni vya lazima kila siku achana na vitu ambavyo haviongezi thamani kwako na kwa watu wengine.

soma zaidi: Mfahamu Vicenti Thomas Lombardi


#3.  KUTOKUWA KITU KINACHO KUSUKUMA
Hakuna kitu ambacho huwa kianfanyika kwa sababu tu kimefanyika. Lazima kuwepo na sababu ya wewe kufanya kitu fulani. Na wewe pia unapaswa kuhakikisha kwamba unakuwa na sababu ya kufanya kitu unachokifanya kila siku. Ile sababu ambayo ilikufanya wewe hapo kuweza kuanza kufanya kitu abacho unakifanya sasa hivi haipaswi kupotea. Kama mpaka sasa hivi hauna sababu ya wewe kufanya kile ambacho unakifanya, basi jiulize kwa nini ulianza? Hii ndio sababu ambayo inapaswa kukusukuma wewe hapo kila siku kuhakikisha kwamba unasonga mbele. Sababu hii itakufanya uweze kuedelea hata kama utakuwa hujisikii kama kuafanya. Je, unayo sababu? Kwa nini unafanya kitu ambacho unafanya sasa hivi?
Tafuta sababu ya wewe kufanya kile ambacho unakifanya sasa hivi.

#4.KUTOWAHUDUMIA WATU
Unaweza kupata kitu chochote kile maishani kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile ambacho wao wanakihitaji. Hii ni kanuni ambayo inatumiwa na watu wengi sana hapa  duniani. Na hawa ni watu ambao wameweza kufikia mbali zaidi katika masuala ya kiuchumi. Matajiri wanachokifanya ni kuhakikisha kwamba wanatafuta namna ya kuwasaidia watu wengine ili waweze kufanikiwa. Kwa kufanya hivi wanajikuta kwamba wao wanaweza kufanikiwa zaidi. Kumbe kitu cha kwanza ambacho kila mwanadamu anapaswa kuhakikisha kwamba anakifahamu maiahani mwake ni kuhakikisha kwamba anawahudumia watu wengine kwanza kabla ya kujifiria yeye mwenyewe. Na mafanikio yatamfuata mbele yake.
#5. NIDHAMU KWA WATU

Mbali na kwamba unapaswa kuhakikisha kwamba unatoa huduma kwa watu ila haupaswi hata siku moja, kutoka na kwenda kwa wat ukiwahuhubiria kwa maneno ya kujidai. Usianze kuwaambia watu, “mnanionaje, mimi ambavyo ninawahudumia na kuwapa maji mtaa huu mzima”? hata kama huduma unayotoa hakuna mwingine anayeitoa,  wala hakuna mtu wa kufikia viwango vyako haupaswi kwenda kwa watu kujidai kwamba wewe ndiwe wewe. Wakubali wengine kwanza, waheshimu na jinyenyekeze kila unapokuwa na watu. Usjikweze, wewe acha watu wengine wakukweze wewe hapo na mambo mengine yatakuja mbele yako. anza safari yako leo. Tukutane kesho kwenye makala nyingine kama hii.
ulikuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
tuwasiliane
0755848391

Ili kupata vitabu vyangu vya KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, na TATIZO si RASILIMALI ZILIZOPOTEA kwa bei ya zawadi ambayo ni sh, 14,000, tuwasiliane kwa nambari 0755848391. au tuma pesa kwenda nambari hiyo hiyo jina GODIUS RWEYONGEZA baada hapo nitumie ujumbe wasapu ili nikutumie.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X