WANAVYOKAMATA NGEDERE NCHINI INDIA (Jifunze Kutoka Kwa Viumbe Hawa)


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako pendwa ya songa mbele. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako una unaenda kujifunza kitu kipya. Wahindi wamebuni njia rahisi sana ya kuwakamata ngedere nchini mwao. Wao wanachofanya ni kuhakikisa kwamba wanachukua mtego na kuweka chakula akipendacho ngedere ndani ya mtego. Mtego huu una uwazi mkubwa sana sehemu ya kuingizia mkono lakini uwazi huu huzidi kupungua kadri unavyokuwa unavyoshuka chini. Hivyo kufanya upitishaji wa mkono ukiwa tupu rahisi sana kama ilivyo kunywa maji lakini kuutoa mkono ukiwa na kitu unakuwa ni mgumu sana. sijui unapata kitu hapo!kwa hiyo ngedere wanachofanya ni kuweka mkono wao kwenye huo mdomo ili kutafuta chakula. Ila kinachotokea ni kwamba mkono huwa hauwezi kutoka humo ukiwa umeshika chakula, mpaka utoe mkono tupu. Sasa uroho wa ngedere akishikilia chakula chake mkononi mwake huwa hapendi kukiachia. Huwa anaendelea kushikilia chakula hicho mpaka pale mwenye mtego huo anakuja na kumkuta. Hali ambayo inamfanya ngedere akamatike kirahisi sana.
Sasa swali haya yote ya ngedere ya nini? Basi sasa hapa tunakuja na somo zuri sana kutoka kwa ndedere hawa,
#1. Tunajifunza kuacha uroho.
#2. Ili kuweza kunasuka katika mtego wa udogo, umasikini, ujinga na  mengineyo basi hakuna budi kuachilia baadhi ya vitu ambavyo si muhimu. Uruhusu mkono wako uachilie vitu kama hivi hapa,
#3. Kufikiri kutatufanya kuwa mabingwa. Nakumbuka shule ya msingi kulikuwa na hadithi iliyokuwa inasema kwamba fikiri kabla ya kutenda. Hali kama hii ndio ambayo tunapaswa kuwa nayo. Watu wengi katika maisha wanashikiliwa na vitu vidogo sana kama ulivyo mtego wa ngedere ila kwa sababu ya kukosa kufikiri basi wanajikuta ni wazembe na hawawezi kunasuka kwenye mtego huo. Acha utani yaani huwezi kunishawishi kwamba umefeli kwa sababu tu ya umeshikiliwa na mtego wa ngedere.
Ulikuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
Jipatie sasa vitabu vyangu kwa shilingi 16,000 tu. Bei ya vkitabu kimoja kimoja ni kama ifuatavyo
1.      KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI tsh.9,000/
2.      TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA ni tsh. 7000/-

Hii ni zawadi ambayo huwezi kuipata sehemu nyimgine duniani. Tuma pesakwaenda namba tajwa hapo juu. Baada ya hapo nipe taarifa ya njia ambayo unapendekeza nikutumie kitabu. Inaweza kuwa ni wasapu, email au telegram. Asante sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X