Habari ya siku hii njema ya leo. Leo ni siku njema sana maishani mwangu, ikiwa ni wiki ya sita tangu mwaka huu umeanza. Hongera sana rafiki yangu kwa hatua unazozidi kupiga
Moja kati ya vitu vinavyopendwa na watu walio wengi sana ni kuangalia tamthiliya. Vijana, watu wazima, na hata wazee. Yaani unakuta watu wanakesha usiku kucha wakiangalia movie. Kuna kazi nyingine hazifanyiki kwa ufasaha kwa sababu ya movie. Kwa mfano unakuta mtoto Wa Kile anapika wakati huo huo anaangalia movie. Sasa movie ikikolea anajisahau hadi chakula kinaungua.
Kiukweli movie zimevutia wengi sana kiasi cha watu kusahau kazi za msingi. Wengine wanadiriki kuangalia movie maofisini. Hii ni hatari zaidi. Maana watu Wa maofisini tunategemea wawe ni watu Wa kutumia ubongo wao kufikiri na kuleta matokeo bora zaidi. Badala yake wanaishia kuangalia movie! Sijui kizazi gani hiki kinatengenezwa!!
Wazazi, walezi, wahusika naomba tusifumbie macho tu jambo hili maana kizazi chetu kinaelekea hatarini. Lakini swali ni nani atamfunga mpaka kengele? Mzazi gani atamwambia mtoto wake aache kuangalia movie wakati yeye mwenyewe ni mtazamaji nambari moja. Au bosi gani atamkemea mfanyakazi wakati na yeye anaangalia movie hizi. Au akiteleza kidogo (asipoangalia) basi anakuwa yu mitandaoni (facebook, unstagram, n.k) anachati!
Utafiti unaonesha kwamba mpaka kijana anahitimu kidato cha sita anakuwa ameangalia movie kwa zaidi ya masaa 20,000. Ndani ya masaa hayo anakuwa ameshuhudia mauaji 15,000, huku akiwa ameangalia vitendo vya ulevi (kuvuta bangi, pombe, n.k) zaidi ya 100,000.
๐๐๐
Hivi ni mtu gani aliandika kitabu hiki cha watu kuangalia movie masaa yote hayo?
Natamani mtafiti afanye utafiti zaidi kwa wanachuo maana na huko vyuoni kuna majipu mengi sana yanayoangalia movie zaidi ya kusoma na kujitengenezea mazingira ya kiutaalam. Natamani utafiti huu uendelee zaidi na kuwafikia wafanyakazi Wa maofisini wanaoangalia movie ili tujue masa mangapi wanayatumia kufanya kazi na ni magapi wanayatumia kuangalia movie.
Itakuwa vyema zaidi utafiti huu pia ukiwafikia watu wazima wakiwa majumbani mwao na watoto wao ili nao tujue wanatumia masaa mangapi kila siku kuangalia movie!
Lakini kwa taarifa hizo za utafiti tuendelee kuchimba kwa undani kidogo maana bado kuna mengi ya kuzungumza hapa;
MPAKA KIJANA ANAHITIMU KUDATO CHA SITA ANAKUWA AMETUMIA MASAA 20,000 KUANGALIA MOVIE!!!!!!!!!!!!!!!!!
Laiti kama masaa haya angeyatumia kuendeleza kipaji chake, basi mpaka anahitimu kidato cha sita angekuwa tayari ni maarufu (word class) kwenye kipaji chake. Maana kuwa worldclass kunachukua masaa 10,000 tu kwa mtu anayeweka juhudi kwenye kile anachofanya. Sasa masaa 20,000 ni mara mbili zaidi.
Kwa maoni yangu, nchi yetu ingekuwa na timu nzuri sana ya taifa ya mpira wa miguu kuliko nchi yoyote kama watu wangeyatumia masaa haya kujinoa kwa ajili ya mpira (hapa nawazungumzia wenye vipaji vya kucheza)
Nchi hii ingekuwa na wasomi wanaoleta matokeo makubwa na wanaofikiria kwa kiwango vha juu sana kama wangeyatumia masaa haya kuhakikisha kwamba wanajiinua na kuendeleza maeneo yao ya kimasomo.
Nchi hii ingekuwa na wafanyabiashara maarufu kama kila mtu angewekeza katika biashara yake ndogo na kuikuza kwa masaa hayo 20,000.
Jambo hili lingepunguza na kuondoa kabisa idadi ya watu ambao hawana ajira maana mpaka mtu anahitimu kidato cha sita angekuwa ameyatumia masaa yake 20,000 ya kwa ajili ya kujijenga kiroho, kimwili, na kiakili.
Hapo sijamgusa mwanachuo! Ambaye Nina hakika mpaka mtu anahitimu chuo basi angekuwa anamiliki kampuni yake.
WATANZANIA ACHENI UTANI,
Mambo ya kuwa kila siku mnasimulia kwamba Messi ni mchezaji mzuri na ana umri mdogo!Yamefikia mwisho, anza kuyatumia masaa yako vizuri kuanzia sasa!
Au mnasema Neymar analingana na mimi kwa umri ila kapiga hatua zaidi yangu achana na nayo. Anza kujijenga, badala ya kuangalia movie masaa yote hayo basi utumie muda huu kujiendeleza Nina hakika siku moja utakuwa kama yeye.
Natengemea miaka michache kutoka sasa hivi nisikie,
NDUNGURU ana miaka 17 ila ni mchezaji maarufu sana na dunia nzima inamfahamu,
CHACHA ni mwimbaji maarufu na umri Wa miaka 21 tu.
Nategemea kusikia MANJI amevunja rekodi ya mbio kwa wakimbiaji marathon.
Nitafurahi pia nikisikia kwamba kijana KOKU (mwenye umri Wa miaka 18) anamiliki kampuni ya kwanza kwa ukubwa barani afrika.
Hili litawezekana kama tutautumia vizuri muda wetu. Badala ya kutumia masaa 20,000 kuangalia movie, tukayatumia kujiendeleza.
MPAKA KIJANA ANAHITIMU KIDATO CHA SITA ANAKUWA AMEANGALIA MATUKIO 15,000 YA UUAJI KWENYE MOVIE!!!!!!!!!!!
Nini? Mpaka kijana anahitimu kidato cha sita anakuwa ameangalia matukio 15,000 ya uuaji kwenye movie. Hahahah! Sicheki kwa sababu ya furaha! Hapa ndipo nakumhuka maneno ya Yesu wakati anasulubiwa msalabani, akina mama walikuwa nyuma yake wakimlilia. Yeye aliwaambia hivi, msinililie mimi, jililie ninyi na watoto wenu. Sasa hapa kila mtu ajililie mwenyewe.
Ngoja kwanza tuongee kitaalam zaidi,
Hivi unafikiri haya matukio ya mauaji wanayoangalia vijana kwenye movie yana mchango kwenye maisha?
Je, mchango huo ni hasi au ni chanya?
Je, mchango huo ni Wa muda mfupi au muda mrefu?
Fikiria zaidi! Fikiria tena! Ebu fikiria kabisaaa! Na chukua hatua!
Kwa maoni yangu,
Kama vijana wataendelea kuangalia na kuona mauaji haya watendelea kuiga na kuishi maisha hayo. Hivyo matendo ya kudhulumu, unyanganyi, wizi na mauaji yataongezeka. Hali kama hii itashusha hadhi yetu sisi kama watanzania.
Soma Zaidi; hii Ndio Siri Iliyonyuma Ya kauli ya Niko Updated!
Lakini pia swali la muhimu la kujiuliza ni Je, tunatengeneza familia za aina gani siku za mbeleni?
WATANZANIA ACHENI UTANI,
Hatuwezi kutengeneza baba na mama bora kwa kuangalia movie, kila wakati. Hapa tutakuwa tunacheza fyongo uwanjani.
Hatuwezi kuwa RAIA wema kwa kushabikia vitendo vya ujambazi tunavyoviona kwenye movie. Tena baada ya kuangalia vijana wengi wanaenda kuweka katika matendo walichokiona! Acha utani, hapa tunacheza kamari mchana kweupee!
MPAKA KIJANA ANAHITIMU KIDATO CHA SITA ANAKUWA AMEANGALIA VITENDO VYA ULEVI 100,000!!!!!!!!!!!!!!
Yaani laki moja kwa kutamkika inaonekana ni rahisi lakini hapa tunapaswa kutafakari sana. Hivi ni vijana wangapi huwa wanaangalia movie na kutoka na somo zuri la kwenda kufanyia kazi, katika hali ya uchanya?
Sasa vijana Wangu changamka?
Kabla ya kunywa pombe kama ambavyo umemwona fulani akinywa kwenye movie basi jiulize kwa nini?
Jiulize faida zake?
Nimegundua vijana wengi wanaona maisha ya kwenye movie ndio maisha haswaaa,,
Sasa lazima tufikirie kwa namna ya tofauti na kuwe na mbadala wa movie. Na kwa kuanzia mbadala Wa movie ni kuhakikisha kila kijana anajua yupo hapa duniani kufaya nini?
Kama lengo letu ni kutengemeza taifa la walevi, basi tuache vitu hivi viendelee. Kama lengo letu ni kuunga mkono uvutaji Wa bangi basi turuhusu movie zaidi za uvutaji ziangaliwe na watoto wetu!
WATANZANIA ACHENI UTANI!!!
Sasa kumekucha nchini Tanzania! Ndio kumekucha! Naamini baada ya hapa kila mtu aliyesoma hapa atachukua hatua madhubuti, kuhakikisha anasonga mbele.
Mimi kazi yangu siku zote ni moja tu! KUUWASHA MOTO! Sasa Nina hakika nimeuwasha moto kwa kiberiti kikichokuwa kimelowa na maji.
Wazazi, walezi, jamii ebu tuliangalie hili kwa jicho la kipekee kabisa.
Mwisho naomba nisamehewe pale nilipotumia lugha ya ambayo utaona kama haijakaa sawa kwako. Sikuwa na jinsi ila kuwasilisha ujumbe kama nilivyouwasilisha.
Unaturuhusiwa kumshirikisha mwenzako bila kuongeza wala kupunguza neno lolote.
Ulikuwa nami
Godius Rweyongeza
0755848391
Sasa unaweza kupata Vitabu vyangu kwa bei rahisi kabisa, yaani kwa tsh. 14,000 tu za kitanzania.
Vitabu hivyo ni TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA (6,000/-)
KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (8,000/-)
Vitabu vyote ni soft copy na vinatumwa kwa njia ya mtandao.
Pesa inalipwa kupitia nambari ya simu, 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA.
Bei ya kitabu kimoja kimoja imeoneshwa hapo juu. Karibu sana.
2 responses to “WATANZANIA ACHENI UTANI, TAMTHILIYA HAZIJENGI”
Namna unavojiweka we mwenyewe na ratiba zako
Dah, asante sana