Hiki Ni Kitu Unchoweza Kufanya Kuyaabisha Makaburi


Kwa siku nyingi sana makaburi ya dunia hii yamekuwa yananufaika sana. makaburi haya yamekuwa yakituibia watu wa aina mbali mbali. yaani yametuibia walimu wazuri ambao hawakuwahi kuwa walimu. Yametuibia wafanyabiashara wazuri ambao hawakuwahi kuwa wafanya biashara, yametuibia maraisi wazuri ambao hawakuwahi kuthubutu hata kuongoza hata kikundi cha watu wawili. Hii ndio kusema kwamba makaburi yameiibia dunia hii kwa karne nyingi sana. makaburini kumejaa miziki mizuri ambayo haijawahi kuchezwa, kumejaa vitabu vingi sana ambavyo haviijawahi kuandikwa, makaburini kumejaa wataalamu wengi sana ambao hawajawahi kuutumia utaalamu wao. Ubora wa makaburi haya huwa hayafuati mtu na kumwimbia. Wizi wa makaburi ni wizi wa kistaarabu sana. yaani makaburi hayakuibii kama wizi mwingine ambao tumewahi kuusikia, makaburi yanakabidhiwa. Japo yanakabidhiwa kitu husika ila bado mimi nauita wizi maana yakichukua ndio yamechukua.

Na imekuwa ni kawaida ya makaburi kwamba watu wanapokufa basi yanakuwa yana uhakika kwamba mtu fulani ambaye anakuja atakuwa na mziki fulani, na mwingine atakuwa na kitu kiingine. Hivyo makaburi yanaiba na kuiba kila siku, kila sekkunde na kila dakika. Ila ukweli ni kwamba unaweza kuyaabisha makaburi. Na njia nzuri sana ya kuyaaibisha makaburi ni kwenda makaburini ukiwa mtupu kabisa. Yaani unaenda makaburini ukiwa ni mtupu kwa asilimia mia moja. kile ambacho makaburi yalikuwa yanategemea kutoka kwako haukitoi wala kuyapa makaburi. Badala yake unahakikisha kwamba kitu hicho umeweza kukitoa kwa watu na kukiacha hapa duniani. Kama ni  mziki basi unahakikisha kwamba mziki huu unauacha hapa duniani na kuwapa watu wafaidike nao. Kama ni kitabu unahakikisha kwamba umekiandka na kukitoa kwa watu ili wakisome, kwa hiyo kabla ya hujaaga dunia hakikisha kwamba unatoa kile ambacho kimo ndani yako. toa kitu hiki na kukitoa kwa watu wengine ili nao waweze kukiona ili utakapokufa uhakikishe kwamba unakufa ukiwa mtupu. Yaani ifikie hatua useme maneno kama ya Paulo kwamba nimeumaliza mwendo, nimevipiga vita vilivyo vizuri, imani yangu nimeilinda. Sasa na wewe hakikisha kwamba unaumaliza mwendo wako vizuri. Piga hatua kila siku kwa kufanya kitu kikubwa na cha ziada. Hakikisha kwamba kila unapopiga hatua unatoa kile kilicho ndani yako. wewe ni zaidi ya ulivyo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X