Huu Ni Muda Mzuri Unaoweza Kukubali Majukumu


Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala haya kutoka songa mbele blog. Imani yangu kwamba leo umekuwa na siku njema sana. Hongera sana kwa siku hii rafiki yangu. Maana hii ni siku ambayo haitakuja kujtokeza katika maisha yako yote. hakikisha kwamba unaitumia vyema kabisa maana siku kama hii hapa haitakukja kujitokeza maishani mwako.

Siku hii ya leo naomba tunaglie, ni muda gani mzuri wa wewe kukubali majukumu katika maisha yako. Maana kuna wakati watu wengi sana wamekuwa  wakiwarushia watu wengine majjukumu ya maisha. Hii ni kutokana na kwamba watu wanafikiri kwamba serikali au mtu fulani ambaye yuko maeneo fulani ndiye anayehusika na maisha yao hivyo wao hata hawahusiki katika kuhakikisha kwamba wanafanya kazi na kufika kule ambako wanataka kufika katika maisha yao.

soma zaidi hapa; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-133 tatizo ni ukosefu wa nidhamu
 Sasa leo nipo hapa kukwambia kuna muda mzuri sana ambao wewe unaweza kuyakubali majukumu. Na muda huu ndio sasa. Muda huu ndio mzuri kwako kuhakikisha kwamba unakubali majukumu ambayo yanakukabili. Kama ni majukumu ya kuendesha maisha yako bila kumtegemea mtu yoyote basi muda mzuri wa wewe kukubali majumu haya ni sasa hivi. Kama ni kuanza kuwekeza basi hakikisha kwamba unakubali majukumu haya sasa hivi maana hakuna muda mwingine kama sasa hivi. 

Muda mzuri wa kuhakikisha kwamba unakubali majukumu ni sasa hivi rafiki yangu.
Cha kufanya sasa hivi angali ani majukumu gani ambayo ulikuwa unayaogopa maishani mwako, na kuyakubali kuyabeba sasa, maana muda wa kuyabeba ni sasa.

bonyeza hapa kujiunga na kundi la HAZINA YETU TANZANIA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X