Ni Kweli Mbwa Mzee Hafundishwi Mbinu Mpya?


Kuna usemi wa kiingereza unaosema kwamba huwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya.  Watu wanaokubaliana na usemi huu wanaamini kwamba huwezi kujifunza mbinu mpya ukifikisha umri fulani. Watu hawa wanaamini kwamba huwezi kupiga hatua hasa ukishafikia hatua ya uzee katika maisha. Jambo kama hili hapa sio kweli. Ukweli ni kwamba wewe sio mbwa. Inawezekana ikawa ni kweli kwamba mbwa mzee hafundiswi mbinu mpya. Ila wewe sio mbwa. Wewe unaweza kujifunza kitu kipya. Wewe bila kujali umri ulio nao kwa sasa, unapasawa kuhakikisha kwamba unajifunza kitu kipya bila kuogopa maana unaweza. Na huu ndio unapaswa kuwa ni utaratibu wako katika utendaji wako wa kila siku. Yaani hauna siku ambayo unapaswa kuwa na likizo katika kujifunza kwako. Kumbuka kwamba wewe sio mbwa. Hivyo ukisikia mtua ankwambia kwamba huwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya basi wewe jua kwamba anamzungumzia mbwa. Na ya mbwa waaachie mbwa, ila ya binadamu yaache tu yaitwe ya binadamu. Wewe ni zaidi ya ulivyo sasa hivi.
soma zaidi: Mwanafunzi ni Zaidi Ya Mwalimu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X