TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-153 Tatizo hujajua umuhimu wa mitandao ya kijamii


Watu wengi sana kwa sasa wameingia katika wimbi la kulalamika kila wakati kwamba mitandao ya kijamii sio mitandao mizuri , badala yake imeharibu jamii. Wanaosema hivyo wanasisitiza kwamba mitandao hii imeleta upotovu mwingi sana kwa vijana kuliko ambavyo dunia imewahi kushuhudia kwenye zama za nyuma.. hata hivyo watu ambao wanasema hivyo wanasahau kwamba mitandao hii ni mizuri sana na imesaidia dunia kwa kiasi amacho hakijawahi kutokea.
Kwa kuwa wakweli haijawahi kutokea kwamba dunia nzima ikaungwnishwa na kitu kimoja ambacho watu wengi wanatumia kama intaneti na mitandao ya kijamii.
Pia dunia haijawahi kuwa na maarifa mengi sana kama ambavyo kwa sasa hivi dunia hii ina maarifa.
Tukichimba kwa undani zaidi tutagundua kwamba hakuna kipindi katika dunia  hii ambapo mtu alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na watu wa sehemu yoyote ya dunia hii kama ilivyo katika zama hizi za sasa hivi.
Sasa kwa nini watu walio wengi hawazioni faida hizi badala yake wanaona hasi?
Hili ni swali ambalo linaweza likaonekana kwamba ni gumu kulijibu lakini hata hivyo jibu lake ni rahihi sana.
Watu wamefanya maisha kuwa magumu kuliko ambavyo imewahi kutokea kwenye dunia hii. Hilo ndilo jibu rahisi na haraka sana kuliko majibu mengine . Kwa lugha nyingine tunaweza kusema kwamba watu wanakomplicate maisha.
Inawezekana unalalamika kwamba misha ni magumu na mitandao imesababisha! Au ukasema kwamba vijana wa sasa hivi wameharibika, hili sio  kweli na ni kweli. Haahah! Sio kweli kwa sababu suala la kwamba kuharibu jamii halianzii mitandaoni bali linaanzia nyumbani kwa baba na mama! Hii ndio kusema kwamba kama baba na mama watajitahidi kuhakikisha kwamba wanamwelewesha mtoto wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii basi mtoto huyo hatafaidika sana. lakini pia kwa kuwa watoto kwa asilimia kubwa hujifunza kwa kuangalia, basi inakuwa rahisi watoto kuwaiga wazazi wao kile wanacho kifanya. Ndio maana wazungu huwa wana msemo usemao kwamba like father like son. Wakimaanisha, kama alivyo mzazi ndivyo alivyo mtoto wake.
Sio kweli pia, kwa sababu aliyetengeneza inteneti na mitandao ya kijamii hakuwa na wazo la kwamba watu waharibike, bali yeye alilenga kurahisisha  maisha/
Sasa kama wewe unainigia kwenye mitandao hii sio kwa lengo la kujifunza unategemea nini? Badilika bhana.  Jifunze namna nzri ya kuzitumia mitandano hii ya kijamii. Tukutane kwenye mzunguko wa wanamfanikio


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X