TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-161 Tatizo unajishikiza kwenye kuta za dimbwi la maji.


Huwezi kuwa mwogeleaji hodari wakati unaendelea kujishikiza kwenye kuta za swimming pool. Ili uwe mwogeleaji mzuri lazima ukubali kuachia kuta za swimming pool na kuingia kati kati ya maji. Kama utaendelea kushikilia kuta za swimming pool, nakuhakakikishia utaendelea kuwasikia waogeleaji hodari kwenye redio.
Vivyo kwenye hali kawaida ya maisha, kama ambavyo huwezi kuwa mfungaji hodari kwa kukaa nje ya uwanja na kuwaangalia wachezaji hivyo hivyo huwezi kuwa na mafanikio kama utakaa tu nje umeshikilia kuta za swimming poola huku ukitaka kufanikiwa. Kama kuna kitu ambacho unataka kukifikia katika maisha yako, basi chukua hatua sasa. Jitupe majini na uogelee ukifuate. Nenda hatua ya ziada na hakikisha kwamba unakifanya.
Hiyo ndio siri ya mafanikio makubwa sana,
Naam, hiyo ndio siri ya kuwa mwogeleaji hodari
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com
karibua sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X