TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA Tatizo hujaweka ukomo


Ili kitu kiweze kufanyika vizuri na kwa ufasaha wa hali ya juu sana unahitaji kuhakikisha kwamba umewekiwekea ukomo hasa katika kukitenda na kukikamilisha. Usipokuwa na ukomo  katika kutenda utajikuta kwamba utakuwa unafanya hiki na kufanya kile. Utajikuta kwamba unaanza kufanya kitu fulani ila bado hukimalizi kwa sababu hakina ukomo,
Kwani ukomo ni wa nini kwenye malengo yangu? Ukomo wako ni muhimu sana kwenye kutimiza ndoto zako na malengo yako. maana kila mara utakuwa unajua kwamba utakapofikia eneo fulani utapaswa kuwa umekamilisha kitu hicho hivyo kila mara utakuwa unaweka juhudi kuhakikisha kwamba unafanikisha kile ambacho unakifanya.
HASARA ZA KUFANYA VITU BILA YA KUWA NA UKOMO
#1 Utahairisha sana
#2utachukua kila njia
#3 hutajua umefanikisha kitu chako kwa kiasi gani
FAIDA ZA KUWA NA UKOMO
Ni rahisi kujua umefikia wapi katika suala zima la mafanikio
Ni rahisi kujua uongeze nguvu kiasi gani katika kile ambacho unakifanya
Ukomo utakwambia kitu gani ufanye kwa siku hii ya leo ni kitu gani usifanye.
Hivyo hakikisha kwama unakuwa na ukomo katika vitu ambavyo unakuwa uanvifanya kila siku. Iwe ni kazini, ofisini, au nyumbani. Iwe ni malengo au mipango yako yaani wewe hakikisha kwamba kila kitu ambacho unafanya kinakuwa na ukomo katika utendaji wake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X