Vitu Vitatu Vitakavyokufikisha Kwenye Kilele Cha Mafanikio


Habari ya siku hii njema sana ya leo rafiki yangu. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana na unaenda kuweka juhudi kuhakikisha kwamba unaweza kufikia mafanikio makubwa sana.
Kufikia kilele cha mafaniko ni rahisi sana. ni rahisi kwa sababu kuna vitu vichache sana ambavyo unahitaji kuvifahamu na vingine kuvipuuzia. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kati ya vitu 10 ambavyo unafanya kwa siku ni vitu viwili tu, ambavvyo vina umuhimu mkubwa sana. hii ndio kusema kwamba kama utapunguza vitu unavyofanya kila siku itafikia hatua mbapo utakuwa unafurahia mafanikio makubwa sana maishani mwako kwa sababu tu umeweza kufanya vitu vichache vyenye umuhimu mkubwa sana.  yaani kama utaweza kufanya vitu viwili na kupata mafanikio makubwa badala ya vitu kumi huoni kwamba maisha ni rahisi.
Sasa ndani ya siku hii ya leo napenda ufahamu juu ya vitu vitatu ambavyo ni muhimu ili kuweza kukufikisha wewe hapo kwenye kilele cha  mafanikio. Kama utavitumia vitu hivi nina hakika baada ya muda mfupi utakuwa umeweza kupiga hatua kubwa sana.

SOMA ZAIDI; Hatua Tatu Zitakaazo Kutoa Sifuri Mpaka Kileleni

  MAZOEZI
“Kuna msemo wa kiingereza ambao unasema kwamba practice makes perfect” ukimaanisha kwamba mazoezi ndiyo hukufanya kuwa vyema. Hii ndiokusema kwamba katika jambo lolote ambalo ungependa kufanikiwa katika maisha yako basi huna budi kuhakikisha kwamba unafanya mazoezi kila siku. Yaani hata kama ni mazoezi katika udogo wake ila hakikisha kwamba unayafanya. Maana mazoezi ndiyo hukufanya wewe kuwa kama ulivyo.
Fuatilia wachezaji wa mpira wazuri Utagundua kwamba wanafanya mazoezi ambayoni makubwa sana huko nyuma ya pazia ambayo wengine huwa hatuyaoni ndio maana muda mwingine huwa inakuwa rahisi kwa watu kusema kwamba fulani kabahatika. Ila kumbe siri iliyonyuma yake ni mazoezi. Hivyo rafiki yangu, hakikisha kwamba unafanya mazoezi juu ya kile ambacho unafanya kila siku.
2.      UVUMILIVU.
Hakuna kitu ambacho huwa kinafanyika kwa wakati mmoja na kuweza kufanikiwa. Hivyo unahitaji kuhakikisha kwamba unavumilia kiasi cha kutosha. Usiache kufanya kile ambacho unapaswa kufanya hata siku moja. Ione kila siku kama siku mpya ya wewe kwenda kufanya kazi zako kwa juhudi kubwa ambayo itakufanikisha wewe kuweza kufikisha mafanikio makubwa sana maishani mwako.
3.      MAONO
Hakuna mtu yeyote ambaye atakuwa na uwezo wa kukuzuia wewe hapo kuweza kufikia hatua kubwa sana maishani mwako kama wewe mwenyewe utakuwa na malengo na  mipango mikubwa sana ya kimaisha. Kama utakuwa unajua unaenda wapi na kwa nini unaenda huko.
Kwa hiyo unapaswa kuwa na maono na malengo ambayo yanakuelekeza ni wapi unaenda na kwa nini unaenda huko. Kwa hakika utaweza kufika katika kilele cha mafanikio.
Tukutane kileleni.
NDIMI.
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio!!

BONYEZA HAPA ILI KUJIUNGA NA KUNDI LA HAZINA YETU TANZANIA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X