A NOTE FROM SONGA MBELE; GO STRAIGHT TO THE POINT


Mara nyingi sana watu wanapokuwa wanaongea na mtu wanaanza kuongea mbwembwe kibao kabla ya kuongea jambo la msingi. Unakuta mtu ana bidhaa anaanza kuzungumzia hili na kuzungumzia lile badala ya kumwambia mtu kwamba ana bidhaa fulani.

Soma Zaidi;  A NOTE FROM SONGAMBELE; TOA KINACHOHITAJIKA

Au mtu anakupigia simu ana shida, anaanza kupiga stori za juzi. Mara anakumbushia mambo yaliyotokea kidato cha tatu.
Jambo kama hili unaweza kulitumia kwa baadhi ya watu likafanikiwa, lakini kwa wengine halitafanikiwa. Maana wengine mkishaongea sana wanaanza kupoteza umakini wa kukusikiliza. Hivyo utajikuta hata haupati kile unachohitaji.

Mambo ya kuzingatia

Hakuna mtu ambaye yupo interested na stori zako. Badala yake waambie kile ambacho unataka kuwaambia.
Kama una bidhaa waambie ninauza bidhaa ABC na itakusaidia 123.

Siku zote penda kwenda kwenye jambo la msingi.

Hata unapochati na mtu. Usitume jumbe zaidi ya tano kabla ya kusema unachotaka kutoka kwake.

Binafsi ujumbe wangu   kwanza na wa tatu ndio huwa umebeba kile nilichonacho moyoni.

Ukiona nimekutumia jumbe zaidi ya tatu na tunajibizana, nikiwa sijakwambia kitu cha msingi. Basi hapo ujue siku  hiyo nimeamua tu kuchati. La sivyo ujumbe wangu wa kwanza, na mara nyingi sana, wa pili huwa unabeba mada ya msingi.

This is a note from songambele


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X