A NOTE FROM SONGAMBELE; Matumizi Ya Pesa


Moja kati ya vitu unavyopaswa kuviepuka ni watu kujua kwamba una pesa.

Yaani hakipaswi kuwepo kipindi ambacho ukishika pesa mkononi kila mtu anajua. Kwa mfano pale unapopokea mshahara. Sio lazima kila mtu ajue kwamba sasa mshahara umeingia.

Na ili kuepuka hili kuna tabia utapaswa kuzibadili.
Mfano sio lazima watu wakujue kwamba unapokuwa na pesa ndipo unapost sana Instagram ukiwa maeneo ya kula bata.

Au sio lazima watu wajue kwamba ukiwa na pesa baasi ndio nguo mpya zinanunuliwa.


Wewe endelea kuishi maisha yako uwe na pesa au usiwe na pesa maisha yako yasitabilike.

Kwa kufanya hivi utapunguza hata wale marafiki ambao huwa wanakuja kwako jua likiwaka na kuondoka jua likizama.

Lakini pia utakuwa umepunguza (au kuwaondoa kabisa) wale wanaokupigia simu kukuomba pesa baada ya kuona umeenda beach, au hoteli fulani.

This is a note from songambele.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

Asante.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X