Je, kuna kitu ambacho ungependa kuona kimefanyika?
Je, kuna kitabu ambacho unafikiri bado hakijaandikwa?
Je, kuna wimbo ambao unajua wazi haujaibwa?
Soma Zaidi; Vitu Vinne (04) Vinavyowafanya Waajiriwa Kuendelea Kuajiriwa
Rafiki yangu kama unajua kuna kitu ambacho hakijafanyika na ungependa kuona kinafanyika, basi weka juhudi kuhakikisha kwamba kitu hicho kinafanyika. Na unakifanya wewe.
Kitu chochote ambacho unapenda kuona kimefanyika, nenda hatua ta ziada na kifanye wewe.
Hivyo kama kuna kazi ambayo unaona haijafanywa kama ambavyo ungependa kuona kimefanyika basi nenda hatua ya ziada, kaifanye.
Kama kuna kitabu ambacho unajua hakijaandikwa basi kakiandike.
Kama kuna ubunifu fulani ambao unajua haujawahi kufanyika basi jua kwamba umekusubiri wewe.
Siku zote kile ambacho unaona hakijafanyika basi nenda hatua ya ziada na kifanye wewe hapo.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391