Haya Ni Malalamishi Unayopaswa Kuwa Nayo


Habari ya siku hii njema sana ya leo rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii njema sana ya leo.

Katika hali ya kawaida watu wanapenda kulalamika.  Wanapenda kuilalamikia serikali kwa sababu ya kutotoa fursa. Wanalalamikia serikali kwa kutowajali. Wanailalamikia serikali kwa kutotoa ajira na malalmishi mengine sana.

Soma Zaidi; Hizi Ni Sauti Tano Ambazo Hupaswi Kuzisikiliza

Kiukweli malalamiahi haya haya hayajengi. Wala hayamfanyi MTU zaidi kuasonga mbele. Badala yake yanamfsnya mtu azidi kupoteza muda na kupoteza muda.

Lakini kuna  malalamishi mazuri ambayo kila mtu anaweza kuwa nayo. Na malalamishi hayo sio mengine Bali malalamishi ya kufanya kitu kizuri zaidi haswa  unapoona mtu kafanya kitu ambacho hujapendezwa nacho.

Kama mtu katengeneza shati kwa mshono ambao hauupendi, usilalamike kwa kusema fundi Fulani ni tapeli. Maana bidhaa zake hazikidhi viwango.

 Badala take katengeneze shati wewe mwenyewe kwa ubora unaoutaka.

Kama kampuni ya simu inatengeneza simu ambazo huzihutaji, basi katengeneze za kwako ambazo ungependa kuziona. Kiukweli hii ni njia nzuri ya wewe kulalamika.

Itumie hii itakufanya usonge mbele.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X