Hii Ni sentensi Ambayo Unahitaji Kuiepuka


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii njema ya leo.

Ndani ya kila siku mpya kuna vitu vya kufanya. Yaani kuanzia asubuhi mpaka ileee jioni unakuwa vitu kibao vya kufanya. Mbali na kwamba unakuwa na vitu hivi vingi sana vya kufanya. Bado unahitaji kufanya uchaguzi na kufanya baadhi na kuachana na baadhi. Huu ndio ukweli. Maana kama ilivyo kweli kwamba ukienda dukani unakuta vitu vingi sana vya kununua ila hununui vyote, badala yake unachagua vichache.

 Vivyo hivyo kwenye chakula, unapoenda hotelini, hununui kila chakula na kukila. Badala yake unachagua baadhi ya vyakula na kuvila. Sasa hii pia ipo kwenye vitu vya kawaida ambavyo unapaswa kuvifanya kila siku.

Lakini kwa leo ningependa uijue sentensi moja muhimu sana ambayo unapaswa kuiepuka kila kunapokucha.

Najua kwamba kila siku unakuwa na mengi sana ya kuongea ila sentensi hii iepuke.

Na sentensi hii sio nyingine. Bali ni sentensi ya haiwezekani.

Kamwe, kamwe, kamwe usiseme kwamba haiwezekani.

Kitu kikubwa sana ambacho kinanishangaza hapa duniani ni kwamba kila unaposema haiwezekani papo hapo unakatizwa na mtu  ambaye anafanya kile ambacho ulisema hakiwezakani.

Soma Zaidi; Hii Ni Sentensi Iliyonichekesha

Hivyo badala ya wewe kusema haiwezekani. Nguvu hiyo iwekeze katika kuangalia ni kwa jinsi gani unaweza kubadili vitu na kuvifanya kuwa bora zaidi  ni kwa namna gani unaweza kuvifanya viwezekane.

 Rafiki yangu, tafuta uwezekano kila wakati.
Hakuna kisichowezekana.

Kila mara unapoona kama vile haiwezekani basi jiulize

Je, kuna mtu ambaye amewahi kufanya kitu kama hiki hapa?
Kama kweli kuna mtu ambaye amewahi kufanya  kitu kama hiki na kufanikiwa, basi na wewe unaweza kufanikiwa katika hilo.

Kama hakuna mtu ambaye hajawahi kufanya kitu kama hicho basi wewe ndiwe wa kwanza. Usiache sasa, endelea kusonga mbele. Yaani wewe ndiwe utakuwa wa kwanza. Na wewe kama mtu wa kwanza basi hupaswi kuacha kufanya kitu hiki hapa…

Inawezekana.

Hahahah! Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X