Katika safari nzima ya kutoka sifuri kuelekea kileleni kati ya vitu ambavyo huwezi kuviepuka ni changamoto na vikwazo.
Vikwazo vipo,
Changamoto zipo,
Kukata tamaa kupo,
Kukatishwa tamaa kupo,
Kukataliwa kupo,
Yaani ili kuweza kukifikia kilele cha mafanikio ambayo unayataka basi lazima ujue wazi kwamba changamoto zote hizi lazima utakutana nazo tu.
Ila ubora ni kwamba matatizo haya na changamoto sio kitu kama wewe utaonesha UBABE.
Moja kati ya vitu ambavyo huwa vinaonesha ubabe mkubwa sana ni MAJI.
Maji yakiamua kupita sehemu fulani lazima yatapita tu, bila kujali kwamba kuna mwamba, kisiki, au nini? Yataendelea kupita taratibu taratibu.
Inafikia hatua kama kikwazo cha maji ulikuwa ni mwamba basi unalika. Na kukatika bila kulazimishwa.
Inafikia hatua kikwazo kilikuwa ni kisiki kinaoza chenyewe bila kuambiwa.
Kiukweli ubabe wa maji ni mzuri sana na ni ubabe ambao kila mtu anapaswa kuuonesha katika safari nzima ya kuelekea kileleni.
Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA