KHERI YA PASAKA RAFIKI YANGU


Habari ya hii njema sana rafiki yangu. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako.

Nachukua nafasi hii nzuri sana kukupongeza kwa nafasi hii ya pasaka leo, rafiki yangu. Hongera sana.

Kama ilivyo kawaida rafiki yangu katika kila tukio linalotokea katika maisha yetu inakuwa ni nafasi bora ya kujifunza. Leo hii pia ikiwa ni pasaka ninaamini kwamba leo hii unayo mengi sana ya kujifunza kutoka kwenye siku hii ya leo.
Hii haijalishi kwamba wewe ni mkristo, mwislamu, mbudha au mtu wa dini gani.

Ila wewe kama mwanamafanikio unaweza kunifunza kitu kikubwa sana kutokana na mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo. Hapa na wewe pia unaweza kuona kwamba mafanikio pia hayaji hivi hivi, il kuna vitu vikubwa sana ambavyo sharti vifanyike kwanza huku nyuma ya ushindi. Na vitu hivi vinaweza kuwa kama ambavyo vilimpata Yesu, yaani kuteswa, kufa na baadae akaweza kuufikia ushindi mkubwa sana. Yaani kufufuka.

Kiukweli ndani ya siku hii ya leo haupaswi kuishia tu kunywa, kubadilisha mlo na kwenda kutembea beach. Toa somo kubwa sana hapa.

Amua kuchukua hatua itakayobadili maisha yako.

Kwa kumalizia kipengele hiki, naomba nikuulize maswali yafuatayo.
Je, wewe siku ya leo unaichukuliaje?
Utafanya nini leo?
Kwa nini utafanya hivyo?
Kitu gani unajifunza kutokana na siku hii leo?
Je, unaweza kukitumia kwenye maisha yako ya kila siku?

Chukua hatua sasa,
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio.

ZAWADI YA PASAKA KWAKO
Rafiki yangu, siku hii ya leo nimekuandalia zawadi ya vitabu viwili.
Ambavyo ni TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kwa sh 16,000 tu. Lipia sasa, kwenda 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie email yako. Utapata kitabu muda kidogo baada ya wewe kutuma pesa. Bei ya kitabu kimojawapo kwa zawadi ya leo ni 8,000 tu. Karibu sana.
Akhsante.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X