Maajabu Ya Vitu Vidogo Vidogo


Haba na haba hujaza kibaba ni maneno ya wahenga. Sijui aliyesema maneno haya akikuwa anafikiria nini hapo mwanzo lakini haya ni maneno ambayo yanafurahisaha sana na yana ukweli mkubwa sana ndani yake.

Siku zote vitu vidogo vidogo ndivyo huchangia vitu vikubwa.

Mara ngingi sana watu huwa wanadharau vitu vidogo vidogo ila ni vitu hivi hivi ambavyo mwisho wa siku huwa vinachangia kitu kikubwa sana.

Huwezi amini meli huwa inazama si kwa sababu ipo kwenye maji marefu sana na mengi bali kwa sababu tundu dogo limejitokeza na linapitisha maji.

Sasa katika maisha yetu ya kila siku. Watu wanazidi kuwa masikini si kwa sababu hawajapata kipato kikubwa sana cha kutosheleza mahitaji yao.bali watu ni masikini kwa sababu tu hawatunzi kile kidogo ambacho kinaingia mfukoni mwao.

Rafiki yangu kama unataka kupiga hatua kubwa sana maishani basi uwe tayari kuweka jicho la ziada kwenye mambo madogo madogo kila siku. Na hapa nina orodha ya mambo madogo madogo bayo unahitaji kuhakikisha kwamba umeyawekea nguvu na juhudi kubwa sana..

Soma Zaidi;  JINSI YA KUONGEZA UFANISI KAZINI-3

1.  MUDA
Kila siku unayo masaa 24 ya kuishi. Unaweza kuamua kuyatumia vizuri au kuacha. Na kwa kawaida muda hujengwa na sekunde moja.
Kama hutumii vizuri sekunde ambayo inakuja mbele yako ndio ujue kwamba inaenda hivyo. Usipojua umuhimu wa sekunde ambayo ni kipimo kidogo kabisa muda jua kwamba itakuwa vigumu sana kuujua umuhimu wa saa, siku, wiki au mwezi. Anza na muda kidogo sana ambao unao sasa hivi kuutumia vizuri utashangaa unapata masaa mengi zaidi kwenye maisha yako.

Siku muda upo tena wa kutosha, ila matumizi.

Mimi ninaaamini kwamba ukiufahamu umuhimu wa sekunde moja utakuwa umefahamu umuhimu wa dakika
Ukifahamu umuhimu wa dakika utakuwa umefahamu umuhimu wa saa.
Ukiufahamu umuhimu wa saa utakuwa umefahamu umuhimu wa siku
Na ukiufahamu umuhimu wa siku utafahamu umuhimu wa wiki.
Ukiufahamu umuhimu wa wiki utakuwa umefahamu umuhimu wa mwezi
Ukifahamu umuhimu wa mwezi utakuwa umefahamu umuhimu wa mwaka.

Mambo madogo madogo huepelekea mambo makubwa sana.

2.  MATENDO
kuna watu wanashangaza sana, yaani wanasubiri mwishoni mwa mwaka ndio wapate mafanikio makubwa sana. Yaani inashangaza kwamba mtu unalala mwaka mzima lakini mwisho wa mwaka ndipo unakuja kusubiri upate mafanikio makubwa sana. Mafanikio ya mwaka mzima huwa yanajengwa na kila siku ndani ya mwaka. Ukiidharau siku moja jua kwamba unakuwa unaupoteza mwaka mzima.
Kila ufanyacho leo jua kinachangia matokeo makubwa sana yako ya siku za mbeleni.

Kama wewe utakaa na kusubiri kwamba siku moja ndipo uje kufanikiwa katika mambo mkubwa , utakuwa hauna tofauti na mwanafunzi ambaye anakaa hasomi na kusubiri siku ya mwisho ya mtihani ndipo asome.

Soma Zaidi: Mafunzo Matatu Kutoka Kwa Viwavi
3. PESA
kama una ndoto kuwa tajiri. Na ninajua unayo. Basi huna budi kuhakikisha kila shilingi ambayo inaingia mfukoni mwako unaitumia vyema sana. Ukiweza kutunza vizuri kila senti. Basi nina hakika itafikia hatua kile kidogo unachotunza kitaongezela na kuwa kikubwa sana na utaweza kufanya uwekezaji ambao dunia nzima itakaa na kuushangaa.

Asante sana, fanyia kazi hayo rafiki yangu. Tujutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X