Ni Mwaka Mmoja Sasa Tangu Kitabu Hiki Kiandikwe


Ni mwaka sasa umepita tangu kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kiandikwe. Kitabu hiki nilikiandika mfululizo na kukipangilia kwa mwezi mzima. Na mwezi huu haukuwa mwingine bali ni mwezi wa nne 2017.

Hapo awali kitabu hiki kilikuwa kimeandikwa kwenye daftari. Kama ambavyo inaonekana hapo juu. Baadae mwezi wa tano wa mwaka jana ulikuwa ni mwezi wa kukihamisha na kukiweka kwenye mfumo wa microsoft word.

Mwezi wa sita kuhariri kulianza.

Binafsi nilijua kuhariri kutachukua siku chache sana. Kilichotokea ni kinyume na matarajio yangu.
Maana mwanzoni nilipanga kitabu kitolewe mwezi wa sita  tarehe 15 2017.  lakini siku zilizidi kusogea.
Tarehe 15 ilifika ikabidi nisongeze mbele mpaka tarehe 30. Cha kushangaza mwezi wa sita ulikatika wote. Wa saba ukafuata, wa nane nao ulikatika.
Ndipo mnano tarehe 25 mwezi wa 9 kikatolewa na kusomwa na watu kwa mara ya kwanza katika historia.

FUNZO:
1. Mipango yote haitakwenda kama wewe unavyotarajia siku zote. Kuna nyakati kila kitu kitaenda vyema na kuna nyakati utakutana na changamoto

2. Weka malengo makubwa sana muda wote, yasipo kamilika utapata kujifunza kitu gani kimesababisha na kukirekebisha.

Kuna mengi sana ya kujifunza ila kwa leo inatosha karibu sana.

Kama bado hujasoma kitabu hiki. Leo hii hakikisha unakuwa nacho mikononi mwako.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X