Unawahitaji Watu Ili Kufanikiwa


Moja kati ya vitu ambavyo mara nyingi sana vinakuwa vimesimama nyuma ya ushindi wa watu mbali mbali ni watu. Watu ambao wanakuwa wanakusukuma kuweza kufikia hatua kubwa sana maishani.

Soma Zaidi;  Usikubali Kukosa Namba

Kwa  mfano ukifuatilia wanasiasa wakati wa kampeni utagundua wanawatafuta watu ambao wanakuwa na  ushawishi sana ili wawasaidie kupiga kampeni.

Ukiwaangalia wanamziki huwa wanawatafuta wenzao wenye ushawishi ili kurekodi nyimbo zao.

Kwa hiyo rafiki yangu pia unahitaji watu. Na sio watu wote wanakufaa, hakikisha unakuwa na watu ambao wanakupa msukumo wa wewe kuweza kusonga mbele.
Watu ambao kila mara watakupiga teke la kikufanya usonge mbele sio uanguke chini kabisa.

Je, wewe watu unaoenda kuwatafuta ni akina nani?


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X