Usibadili Kioo


Tunaangalia kwenye kioo tunajiona sisi wenyewe.
Itaonekana ajabu pale utakalalamika kwamba juu ya kile unachokiona kwenye kioo.
Ni ajabu pia kubadili kioo ili upate picha ya tofauti.

Kama tunataka kubadili picha ya kweye kioo lazima tujibadili sisi wenyewe.

Kwa maneno mengine ni kwamba kama hutaki matokeo ya kile unachopata kwenye maisha basi unahitaji unahitaji kujibadili wewe kwanza ndani yako.

Usiweke nguvu katika kutafuta kwa nini wewe umshindwa? Tumia muda mwingi kuangalia ni kwa namna gani kushindwa kwako ni mafanikio tosha.

Maana ukiweka nguvu katika kuangalia kwa nini umeshindwa utaishia kushindwa.
Siku zote lazima upate kile ambacho umewekeza nguvu.

Na sheria ya asili inasema UTAVUNA ULICHOPANDA.
Kumbe kile ambacho unafuatilia sana ndicho unachopanda na ndicho utakachovuna.

Soma Zaidi;  Kioo Hakidanganyi

Kama unataka kuona kitu cha tofauti lazima ufanye uamuzi wa tofauti.

Kumbe unachohitaji hapa ni kuwa wewe mwenyewe.
Mtu pekee ambaye wewe unaweza kuwa ni kuwa wewe mwenyewe.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X