Vitu Haviishi Kama Vilivyoanza


Vitu haviishi kama vilivyoanza
Hapa katikati huwa kuna mabadiliko.
Kazi hubadilika
Marafiki hubadilika
Kipato hubadilika
Mahusiano hubadilika

Kwa hiyo pale utakapoona kitu hakiendi kama ambavyo kimeanza basi hapo usisite kuweka juhudi ili kupata matokeo unayoyataka.

Vitu haviishi kama vilivyoanza.

Watu mara nyingi hupenda kukuona kama walivyokuona siku ya kwanza. Kama hutapiga hatua na kusonga mbele zaidi basi watu watazidi kufurahi na kuona mambo ni super.

 Ila ukipiga hatua ndogo na kubadilika tu, basi hapo hapo watu wataanza kujiuliza kila aina ya maswali. Kama kukusema, basi wataanza kukusema, tena kwa nguvu.

Ila Leo nataka nikwambie kwamba vitu huwa haviishii kama ambavyo huwa vinaanza.

Na wewe hutabaki jinsi ulivyo kama utaweka juhudi.

Rafiki yangu,  wewe kuwa tayari kusababisha mabadiliko sasa hivi


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X