Kuna watu, yaani yeye asipoonesha ka ishara ka kukupinga haridhiki. Yaani hata kama utafanya mambo mazuri lazima yeye atakuwa na kinyume chako.
Yeye furaha yake huja pale anapoonekana amekusema kwa watu wengine.
Furaha yake ni kuona doa kwako.
Furaha yake ni kwamba wewe urudi chini na yeye apande juu.
Yeye anajua njia moja ya kufanikiwa. Na yenyewe ni kumvuta mwezako na kumwangusha chini.
Soma Zaidi; Huyu Ni Mtu Ambaye Unapaswa Kumwepuka
Rafiki yangu, achana na hawa wajinga. Binafsi nawaita wajinga maana hawajui walifanyalo. Hawakujui wewe ni nani.
Achana na hawa wajinga. Kila wapokukatisha tamaa, simama wima. Fanya mara kumi zaidi kile wanachikukatisha tamaa.
Kila wanapokuvuta, simama wima fanya mara kumi zaidi kile wanachokuvuta wewe urudi nnyuma.
Usibishane nao, utapoteza nguvu bure. Maana wao wanapenda kuona hilo.
Usiwalaumu, wewe utakuwa mjinga kama wao.
Usiwakasirikie maana una mengi sana ya kufanya.
Ukikutana nao cheka, na songambele. Usikae na kuanza kuwafikiri. Usiwape nafasi, yaani wasahau mara moja, sahau, sahau.
Mwisho tambua kwamba wanafanya wasilolijua hivyo wachukulie kama watoto wadogo.
Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
Hahahah! Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA