Haya Ni Mambo Manne (04) Ambayo Unapaswa Kuyafanya Asubuhi


Kila siku mpya huwa inaanza asubuhi. Kila asubuhi huwa ni mpya. Uwezo wa kuipata na kuishi ndani ya asubuhi mpya ni jambo jema sana. Kwa hiyo kila siku kunapokucha lazima ujitahidi kuhakijisha kwamba unaitumia vyema asubuhi yako.

Kuna mambo manne (04) ambayo unaweza kuyafanya kila unapoamka asubuhi.
Na mambo haya ni kama ifutavyo.

1. KUSHUKURU.
Neno la shukrani unapoamka asubuhi ni neno la maana sana. Hakikisha kwamba asubuhi unashukuru Muumba wako kwa kukujalia siku nyingine. Kumbuka wakati wewe unafurahia maisha ndani ya siku mpya kuna watu hawana uwezo wa kushukuru kama wewe.

Kushukuru ni kuomba tena, huu ni usemi wa wahenga. Hivyo kama utaamka asubuhi basi hakikikisha kwamba umeshukuru tena, basi utaweza kuiendea siku yako kwa ubora sana.

2. TOKA NJE NA VUTA PUMZI KWA NGUVU.
Unapokuwa umelala, mfumo wako wa utendaji kazi katika mwili unakuwa umepumzisha baadhi ya kazi. Mfumo wa mzunguko wa damu pia unakuwa umepunguzwa na kutoa damu kidogo kwa baadhi ya maeneo ya mwili wako ili uweze kulala kwa raha msatarehe. Hivyo unapoamka hakikisha unavuta pumzi kwa nguvu ili kuweza kuupa mwili wako nguvu ya kusukuma damu. Lakini pia ili uweze kuanza kazi kwa kasi mara moja ndani ya siku yako.

Soma Zaidi: Njia Tano (05) Za Uhakika Za Kupoteza Muda

3. KUNYWA MAJI YA UVUGU VUGU
Sambamba na kuvuta pumzi kwa nguvu, unahitaji pia kunywa maji ya uvuguvugu. Kazi ya maji ya uvuguvugu pia ni kuuchangamsha mwili, lakini pia ni sehemu ya kifungua kinywa chako.

Kitaalamu pia inashauriwa kunywa maji glasi nane kwa siku. Hivyo unapokunywa glasi moja baada ya kuamka, hiyo inakuwa ni sehemu ya glasi nane za siku hiyo.

4. PATA MWANGA WA JUA
Je, unajua kwamba mwanga wa jua ni muhimu sana? Je, umuhimu wake ni upi?
Naam, mwanga wa jua ni muhimu, muhimu sana kwa kila siku yako.
Kwa kawaida mwili wa binadamu umezoea kwamba  unapokuwa katika giza unapaswa kulala. Sasa ili kuuondoa katika hali ya kulala mwili wako, utapaswa kuhakikisha umeuleta kwenye mwanga wa jua. Jambo hili dogo litakuongezea ufanisi kwenye kazi zako zaidi ya kawaida.

Haya ndio mambo manne ambayo hupaswi kuyasahu kila uamkapo asubuhi.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X