Hii Ni Kazi Kubwa Unayoweza Kujibebesha


Kama kawaida kila siku huwa nasisitiza umuhimu wa kazi. Na kila mara ninapokutana na mtu kitu kikubwa ambacho huwa sifichi huwa ni umuhimu wa kazi. Na jambo hili huwa nalisema au kwa maneno au kwa vitendo.

Wakati wa utendaji wa kazi unapaswa kufahamu kwamba kuna kazi za muhimu na kazi ambazo sio za muhimu.

Lakini pia kuna kazi ambazo unajibebesha.
Kazi hizi za kujibebesha hazina umuhimu kwako na hazikufai. Yaani unazifanya ila zinakupunguzia nguvu zako kitu kinachokufanya ufike jioni ukiwa umechoka na bila ya kuwa na nguvu. Kwa hakika kama utaendelea kufanya kazi hizi utazidi kupoteza nguvu zako. Ila ubora leo hii umesoma hapa, basi nina hakika utabadilika na kuanza kuchukua hatua. Na kazi hizi sio nyingine bali ni kazi za

 1. KUFUATILIA MAISHA YA WATU WENGINE.

Je, umejiajiri kufanya kazi hii. Je, unatumia muda wako kiwakosoa watu wengine. Kama.unafanya hivi jia kwamba unapoteza muda wako. Badilika sasa uanze kutumia muda mwingi katika kufanya kazi za maana na zinazokujenga. Anza kujifuatilia wewe mwenyewe. Kama wewe binafsi huwezi kujifuatilia unataka mtu gani akufuatilie?
Achana na maisha ya watu wengine, jifuatilie wewe mwenyewe.

Soma Zaidi; Vitu Vinne Vinavyowafanya Waajiriwa Waendelee Kuajiriwa
2. KUWAKOSOA WENGINE
Hii ni kazi nyingine ambayo haina maana ambayo umejiajiri kuifanya. Yaani wewe mwanamziki fulani akitoa wimbo wewe unaanza kukosoa angeimba hivi. Mara kaigiza kwa fulani, mara kaiba mwondoko wa fulani. Inakuhusu?
Naona tu unapoteza muda sana.
Unajipa kazi kubwa sana ambayo haina maana.
Badala ya kufanya kazi kama hii hapa, jiajiri kufanya na kutoa kazi zako. Sababisha watu wakuongelee wewe. Sio wewe ukae uwaongelee watu wengine. Kumbuka kwamba kufanikiwa ni juu yako. Kushindwa pia ni juu yako.
Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X