Hivi Ndivyo Unaweza Kupata Muda Zaidi Wa Kazi Zako


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo.

Kila siku una masaa  24 ya kuishi. Masaa 24 ya kufanya kile unachopaswa kufanya masaa 24 ya kufanya kila kitu.
Je, unapata muda wa kufanya kazi za muhimu kwako?
Unaweza kupata muda wa kufanya kazi yoyote ile ambayo unataka kama utaamua.

Suala zima la kwamba hauna muda wa kufanya kitu fulani ni kwa sababu kile kitu hujakiweka kwenye vipaumbele vyako. Kitu kikubwa sana ambacho unaweza kufanya sasa hivi, ni kuainisha vipaumbele vyako. Na kuhakikisha vile vitu vya msingi ambavyo unapaswa kuvifanya unavipa kipaumbele na unahakikisha unavifanya kila siku. Ni ksa jinsi hii utapata muda zaidi ndani ya siku yako.

Rafiki yangu kafanyie kazi hili siku hii ya leo.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X