Kosa Kuu Ambalo Watu Hufanya Wakati Wa Kuweka Malengo


Habari ya siku hii njema sana rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako na unaenda kufanya mambo makubwa sana ndani ya siku hii ya leo.

Kiukweli siku hii ya leo ni siku ambapo wewe hapo unapaswa kufanya makubwa sana.
Na haya makubwa utayafanya kama tu utakuwa na malengo? Je, unayo? Malengo yako ni yapi? Je, malengo yako uliyaweka mwanzoni mwa mwaka huu? Je, umefikia wapi? Je malengo yanakwambia leo utafanya nini?

Kama mwanzoni mwa mwaka huu uliweka malengo au kama hukuweka malengo ila upo kwenye mpango wa kuweka malengo makubwa sana mwaka huu basi leo hii ninapenda kukwambia kwamba kuna kosa   ambalo watu huwa wanafanya katika kuweka malengo.
Makosa hili ni

 Kuweka malengo madogo sana.
Kutokana na ukweli kwamba watu walio wengi hawapendi kuambiwa kwamba watashindwa, wala hawapendi kuambiwa habari za kwamba malengo yao hayafikiki. Hivyo watu hawa hujitahidi kuweka malengo madogo sana.
Soma Zaidi; Haya Ni Malalamishi Unayopaswa Kuwa Nayo
UKWELI ULIPO LALA: Malengo yako yanapaswa kuwa makubwa sana.  yaani kiufupi ni kwamba kama sasa hivi umeweka malengo fulani, basi unapaswa kuyazidisha mara kumi zaidi.

 Malengo yako yanapaswa kuwa mara kumi zaidi ya sasa.

Kama una lengo la kuingiza kipato cha ziada cha laki moja kwa mwezi basi wewe weka malengo mara kumi zaidi. Yaani weka malengo ya laki mara kumi ambayo ni sawa na milioni moja.

Kiuwekweli ukifanya hivi utakuwa umepiga hatua kubwa sana katika suala zima la uwekaji wa malengo.

Kazi ya kufanya siku hii ya leo. Zidisha malengo mara kumi zaidi ya yale uliyonayo sasa hivi. Na anza kuyafanyia kazi. Yaani ongeza juhudi mara kumi zaidi.

Kama umeweka lengo la kupata maksi mara kumi zaidi, basi soma mara kumi zaidi.
Kama umeweka lengo la kuongeza kipato mara kumi zaidi, basi tafuta mbinu za kuongeza kipato mara kumi zaidi.

Ni kwa jinsi hii utaweza kufanya makubwa sana katika safari yako ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X