Swali Muhimu Unalopaswa Kujiuliza Kabla Ya Kulala?


Binadamu yeyote amezaliwa na kupewa kazi maalum ya kuja kushughulika nayo hapa duniani. Kazi hii kama utaifanya na kuitimiza kila siku itakufanya ujisikie huru, lakini pia itawafanya watu  unaoishi nao karibu wafurahie maisha. Kiufupi ni kwamba hujaishi siku ya leo kama hujafanya tendo na kuongeza thamani kwa mtu.

Usishangae, najua umezoea kila siku unapenda kufanya vitu vya kwako kwako tu bila kuwajali watu wengine. Ila ukweli ni kwamba kama unataka kufurahia maisha wasaidie watu kwanza utafurahi sana.

Ukiangalia watu wa mabenki kama CRDB, wanakusaidia wewe kutunza pesa. Lakini pia wanakusaidia wewe kutoa pesa kwa njia rahisi sana. Na kwa namna hiyo wao wanalipwa.

Kazi yankusaidia watu ni ya kila mtu. Kama ulikuwa bado hujafikira kuwasaidia watu anza kufikiri kuanzia leo. Mmoja wa waandishi maarufu na wajasiliamali maarufu anayejulikana kama Zig Ziglar aliwahi kunukuliwa akisema kwamba utapata chochote unachohitaji kama utawasaidia watu wengine kupata wanachohitaji.

Soma Zaidi; Usikubali Kukosa Namba

Kama swali lako ni je, nitapata nini kwenye kuwasaidia watu wengine
1. Utapata unachohitaji kama utawasaidia watu kupata kile unachohitaji.

2. Utaishi maisha yenye furaha

3. Utagusa maisha ya watu wengine.

Swali la kujiuliza siku ya leo, nimemsaidia nini mtu anayeishi kwenye dunia hii.
Kama hujafanya hivyo usilale, fanya kitu kidogo cha kuwasaidia watu wengine.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X