Kila siku mpya inakuja na mambo mapya. Ndani ya kila siku mpya tunakutana na watu wapya. Kila mtu ana mchango wake katika kuhakikisha sisi tunasonga mbele. Usisahau kushukuru. Usisahau kushukuru kile ambacho watu wanakufanyia.
Kuna watu ambao wanaweza kukuzuia wewe kufanya kitu fulani, ila mara ukakaa na kufikiri na kuja na mbinu mpya. usisahau kuwashukuru maana wamekupa mwanya wa kukua.
Kila changamoto unayokutana nayo, baada ya kuimaliza itakuwa imekuimarisha na kukufanyakuwa bora zaidi. Usisahu kushukuru kwamba umeipita salama.
Jenga utaratibu wa kushukuru kila siku.
Shukuru kwa watu uliokutana nao.
Shukuru kwa marafiki zako.
Shukuru kwa sababu unavuta pumzi.
Shukuru kwa sababu umepata chakula.
Shukuru kwa sababu wewe ju wewe.
Shukuru, tena na tena.
Asante sana kwa kusoma makala haya. Nakutakia utekelezaji mwema.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA