Je, nitawezaje kuwa na kesho bora? Nifanyeje ili niweze kuiboresha kesho kuwa bora? Nifanyeje ili niwe na maisha mazuri? Haya ni baadhi ya maswali ambayo huulizwa na watu walio wengi sana. wakitaka kujua kama wanaweza kutoboa katika maisha. Ukweli ni kwamba kila mtu anaweza kutoboa na kufikia hatua kubwa sana. Lakini je upo tayari.
Kuna vitu ambavyo unapaswa kuvifanya leo ili uweze kutengeneza kesho bora.
Soma Zaidi: Hivi Ndivyo Unavyoweza Kusoma Kitabu Kwa Wiki (Mbinu Nne Za Uhakika)
1. KUWA NA MALENGO.
Moja kati ya vitu ambavyo vinafanya kazi ni malengo. Lakini uliza ni watu wangapi ambao wana malengo. Utashangaa, ni wachache, wachache sana. Kwa nini? Kwa sababu malengo yanahitaji ulipe gharama. Malengo yanakupa picha ya vitu vijavyo na jinsi vinavyofurahisha, ila kuvifikia lazima uwe tayari kulipa gharama.
Upo tayari?
2. KAZI, KAZI, KAZI.
Kati ya vitu ambavyo huwezi kuviepuka ili kufikia malengo makubwa sana maishani mwako ni kufanya kazi. Iwe lengo lako ni kuwa mjasiliamali, au ni kuwa mwajiriwa atakayepandishwa vyeo mara kwa mara basi lazima uwe tayari kufanya kazi kwa bidii. Tena kaa bidii sana.
Kwa leo fanya haya ili uweze kuyafikia yajayo ambayo
Yanafurahisha, ila lipa gharama.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391