Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo.
Karibu sana tupate kujifunza kitu kipya kwenye maisha yetu.
Ukikutana na watu wengi sana utawasikia wakisema, ukitaka kupata hiki au kile basi fanya hivi. Lakini watu hawa ukiwafuatilia kwa ukaribu utagundua kwamba hawafanyi kile wanachokiongea.
Watu wanajua kila kitu na kila sheria inayofanya kazi, ila sasa kazi ni kuiweka sheria hiyo katika matendo.
Sio kitu kigeni kusikia mtu anasema fanya biashara fulani. Au ukifanya hivi au vile basi biashara yako itapendeza sana.
Soma zaidi; Maisha Unayaonaje-1?
Sio kitu kigeni pia kusikia mashabiki wakisema kwamba kama mchezaji fulani angecheza hivi basi angefunga goli. Hii maana yake nini? Maana yake watu wanajua kile kinachofanya kazi na kisichofanya kazi.
Ila tatizo hawaweki kile wanachojua katika matendo.
Rafiki yangu, wewe unapaswa kujitofautisha mwenyewe. Anza kuweka katika matendo kile unachojua kinafanya kazi.
Kama unajua njia nzuri ya kuiinua biashara yako ni kufanya kazi fulani. Basi ifanye ili uone matokeo yake.
Weka katika matendo kile unachofahamu. Matendo yanalipa sana, kuliko maneno. Hivyo kuwa mtu wa matendo badala ya maneno. Usikubali maneno yawe mengi kuliko matendo. Kubalia matendo yako yawe mengi sana kuliko maneno.
Kwa hiyo njia nzuri sana ya kufanya kazi kubwa sana ni kuweka katika matendo kile unachofahamu kinafanya kazi badala ya kuishia kukiongea tu.
Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio