Hiki Ni Kipimo Kinachotumika Kupima Mafanikio Yako


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo. Imani yangu kwamba leo hii ni siku njema sana kwako na unaenda kuweka juhudi kuhakikisha kwamba unafanhya kazi kwa bidii kubwa sana kuhakikisha kwamba unafikia mafanikio makubwa sana. hakika siku hii ya leo usiiache ikaenda hivi hivi tu. Itumie vilivyo kuhakikisha kwamba unaweka utofauti kwenye dunia hii.
Ndani ya siku hii ya leo tujifunze kipimo muhimu sana ambacho kitatumika kupima mafanikio yoyote yale ambayo utayapata kwenye maisha yako. kwanza kabisa naomba ifahamike kwamba uwepo wako hapa duniani ni maalumu sana kwa ajili yako wewe kuhakikisha kwamba unafanya kitu na kukifanikisha.
kitbu hiki kipo kwa ajili yako
Hivyo hauna sababu ya kutofanya kitu na kuhakikisha kwamba umekifanikisha. Wala usianze kusema kwamba Mungu akipenda kitu hiki nitakifanya vizuri. Au usiseme, mimi napanga tu ila Mungu asipoamua siwezi kufanikisha kitu. Hapana hakuna kitu kama hicho. Yaani uwepo wako hapa duniani, ni ishara tosha kwamba Mungu anapenda ufanikiwe.
Pia cha kufahamu ni kwamba Mungu hatakuja na kuanza kukwambia kwamba sasa ni wakati wako wa kufanikiwa rafiki yangu. Hatakuja kukwambia kwamba fanya A, B, C ili ufanikiwe. Ni juu yako kuhakikisha kwamba unafanya kazi kwa bidii sana ukimuhusisha Mungu ili uweze kufanikiwa.
Lakini mafanikio yako yatawezekana kama utafahamu kitu kimoja na kuhakikisha kwamba umekifuata. Mafanikio yako pia yatapimwa kitu hiki hiki. Na hiki sio kitu kingine bali ni HUDUMA ZAKO KWA  JAMII. Hiki ndicho kipimo kikubwa sana cha mafanikio. Kadri unavyotoa zaidi kwa jamii yako ndivyo ambavyo unaweza kupata zaidi na zaidi. Siku zote anayetoa ndiye anayepokea zaidi na zaidi.
SOMA ZAIDI’; Usibadili Kioo
Kama wewe umeijenga akili yako chini ya msingi wa kupokea tu bila kutoa. Itakuwa vigumu sana kupokea. Ili upokee lazima uwe tayari kutoa kwanza. Ndio maana tunashuhudia wafanyabiashara wanawekeza kwanza katika kitu fulani kabla hata hawajaanza kupokea pesa kutoka kwenye kile kitu. Hii ni kkutokana na ukweli kwamba wanaijua sheria hii ya kwamba ili upokee lazima utoe.
Sasa jambo hili lipo kila mahali. Ni sheria kwamba ili upokee lazima utoe kwanza. Na hiki ndicho kipimo cha mafanikio. Kama ni mwanafunzi ili ufanikiwe na upate matunda ya masomo lazima ukubali kuwekeza kwanza kabla ya mavuno.
Kama ni mkulima kabla ya mavuno lazima uwe tayari  kuwekeza gharama kwanza
Kwa mwanasiasa pia ukimwona anag’aa, ujue kuna sehemu kawekeza na kwanza.
Lakini wote hawa  kwa pamoja, tunajua wazi kabisa kwamba wamefuata sheria ya KUTOA KWANZA KABLA YA KUPOKEA. Rafiki yangu, sheria hii ipende na uifuate, maana ni sheria muhimu sana kwenye maisha yako ambayo itakuvuta ba kuweza kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio. Asante sana rafiki yangu na hongera kwa siku hii yaleo. Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X