Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo. Ni siku njema sana kwako na ni siku ya kipekee sana kwako, hiyo hakikisha kwamba hauipotezi siku hii ya leo.
Mara nyingi sana huwa tunapanga maeneo ya kwenda na watu wa kukutana nao. Huwa tunapanga ni muda gani tutakutana na watu husika.
Lakini je, ushawahi kujiuliza ni kitu gani huwa unasahau kwenye mpangilio wa vitu vyako ambavyo unafanya? Je, ni vitu gani hivyo?
Kila unapopanga kukutana na mtu kuna kitu kimoja na cha muhimu sana ambacho huwa unasahau. Na kitu hiki sio kingine bali kupangilia muda ambao utakaa na mtu ambaye unakutana naye. Jambo hili hapa huwa linapelekea watu walio wengi sana kukutana na watu na kupiga soga asubuhi hadi mchana na pengine mpaka jioni. Unakuta mtu wanakutana saa nne wanaongea na kuongea hadi mambo ambayo si ya muhimu lakini wao wanazidi kuongea tu. Saa tano inafika , mara saa sita na kuendelea.
Kwa namna hii hapa watu walio wengi sana huwa wanajikuta wanapoteza muda sana. hivyo rafiki yangu, moja kati ya jambo la muhimu sana kwako ambalo unapaswa kulifahamu ili kuepuka kupoteza muda ni kuhakikisha kwamba unapagilia siku yako siku kwanza unapoamka asubuhi. Hakikisha kwamba unakuwa na ratiba ya kitu gani utafanya, kwa hiyo mtu anapokutana na wewe, na yeye pia anapaswa kuwa kwenye ratiba. Hii ndio kusema kwamba wakati wa majadiliano utakuwa unajuwa wazi kabisa kwamba kuna kazi fulani inafuata ambayo inanihitaji niwepo. Hata stori zikinoga bado utakuwa na ujasiri wa kuzikatiza kwa kusema sasa naenda kufanya kazi fulani. Inanihitaji.
Lakini pia unapokutana na mtu hakikisha kwamba unamwambia kwamba utaongea naye kwa muda fulani. Hali kama hii hapa itakupuguzia wewe kupoteza muda mwingi sana kuongea na mtu na pengine kujikuta kwamba unaongena naye mambo ambayo si ya muhimu sana. lakini pia jambo hili hapa litakuweka litamfanya yule aongee mambo ya msingi na kuachana na mambo ambayo si ya msingi. Na kwa kuwa utakuwa umemwandaa kisaikolojia mapema kwamba una kazi ambayo unapaswa kuifanya. Hali hii haitamstua sana hasa kama mlizoea kuwa mnapiga soga pamoja kila siku.
rafiki yangu kuwa makini sana na muda wako. Hakuna muda wa kupoteza. Hauna hata sekude moja ya wewe kupoteza. Hakikisha kwamba kila sekunde inayokuja kwako unaitumia vyema kabisa. Usikubali kuipoteza hata sekunde moja. Kwamwe usikubali kuipoteza hata sekunde moja. Muda ni muhimu sana, sana, sana. hivyo ulinde muda wako kwa kufanya mambo ya msingi na ya maana sana. karibu sana