Hivi Ndivyo Unaweza Kutengeneza Kazi Inayokonga Mioyo Ya watu


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo.

Hivi ushawahi kuwa na wazo la kufanya kazi kubwa sana maishani mwako? Bila shaka umewahi kuwaza juu ya kuwa mwanamziki mwenye wimbo unaoitwa wimbo wa taifa. Au umewahi kufikiri juu ya kuwa mwandishi atayeandika hadithi itayosomwa na watu wengi na kuwekwa kwenye mtaala wa elimu.

Na ninajua kwamba unawajua baadhi ya watu waliofanya katika maeneo fulani na sasa zinafanya vizuri. Sasa kitu gani huwa kinawafanya watu waweze kutengeneza kazi bora kiasi hicho na wewe ushindwe?

Basi leo hii ninaenda kukuelekeza kwa umakini jinsi unavyoweza kutengeneza kazi itakayokonga nyoyo za watu.

1. UNAPASWA KUWA NA SABABU
Je, kwa nini unataka kutengeneza kazi fulani?
Kwa nini unataka kuimba huo mziki? Kwa nini unataka kuandika hicho kitabu? Basi kumbe unapaswa kuwa na sababu kubwa inayokusuma wewe kufanya hivyo. Sababu hiyo inapaswa kuwa na nguvu kiasi kwamba kila wakati utasukumwa kusonga mbele kufanya kazi hiyo.
Miongoni mwa sababu chache za maana ambazo unaweza kuzitumia ni
Kwa sababu haijawahi kufanyika kazi kama hii hapa.

Kwa sababu mimi nimezaliwa kufanya kazi hii hapa

Kwa sababu nimechoma madaraja yote moto na hivyo sina jinsi, isipokuwa kufanya hii kazi

Hizo ni baadhi ya sababu unazoweza kuwa nazo zikakusaidia kusonga mbele.

Soma Zaidi: KONA YA SONGAMBELE; Hii Ni Kauli Inayodidimiza Ubunifu Barani Afrika

2. FANYA KAZI BORA
Njia nzuri ya kufanya kazi itayokonga nyoyo za watu ni kufanya kazi bora. Fanya kazi bora sana na ya tofauti.

Tofauti kati ya kazi kubwa sana zinazodumu na zinazokonga nyoyo za watu ni kwamba kazi inayokonga nyoyo za watu inajengwa chini ya misingi ya kuchapa kazi, zimepewa muda, nguvu imewekezwa na mateso.

Kama unataka kutengeneza kazi itakayodumu kweli na kukonga nyoyo za watu basi ITENGENEZE KWELI.

3. HUSIKA KATIKA KUIFANYA KAZI
Huwezi kumkodisha mtu wa kukupigia push up. Ni kanuni.

Hakuna mtu anayeweza kuzalisha kazi bora na nzuri kama wewe. Huwezi kumkodi rafiki yako akufanyie kazi bora sana huku wewe ukiwa umekaa kwenye kochi. Kitu pekee unachoweza kufanya ili uwe na kazi itayokonga nyoyo za watu basi ni wewe kuhusika.
Husika mwanzo wa kazi mpaka mwisho.

4. IPE MUDA
Ipe muda kazi unayotaka kuifanya. Usitake ulale usiku uamke asubuhi ufanye ile kazi na jioni yake itoke. Ipe muda, fanya utafiti. Soma zaidi. Wafuatilie watu walioweza kufanya kazi bora zaidi kwenye eneo ambalo na wewe unaenda kulifanyia kazi.

Rafiki yangu, ukizingatia mambo hayo manne nina hakika ukitengeneza kazi itakuwa ya tofauti kabisa.
Karibu sana tuendelee kujifunza kwa pamoja kupitia mtandao huu na kundi la wasapu la HAZINA YETU TANZANIA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X