Hivi ushawahi kujiuliza au kukaa na kufikiri siku ambayo utaingia katika chumba fulani chenye watu wakakaa na kukusikiliza juu ya wazo lako bora lenye maana sana? Au ushawahi kujiuliza ni kwa jinsi gani wazo lako linaweza kukubalika duniani kote?
Kiukweli jibu la swali hili hapa ni rahisi sana. Yaani ni rahisi kama ilivyo kunywa maji. Kama unataka wazo lako likubalike dunia nzima basi huna budi kukaa chini na kuanza kulifanyia kazi. unaona eeh! Yaani ni rahisi sana kiasi hicho hapo. Wazo lolote lile ambalo wewe hapo unalo na unaona kwamba lina manufaa makubwa sana kwa jamii yako, basi kaa chini anza kulifanyia kazi.
Soma Zaidi: Nchi Za Ulimwengu Wa Tatu Au Watu Wa Ulimwengu Wa Tatu? Ipi sahihi?
Ni rahisi sana kusema kwamba mimi nilikuwa na wazo fulani, ningelifanyia kazi leo hii ningekuwa sehemu fulalni. Ni rahisi sana, ila wewe unachohitaji sio kuongea mbele ya watu ili uonekane kwamba na wewe una mawazo ya kujenga. Unachohitaji ni wewe kuingia kwenye ulingo wa kufanya vitu na kuhakikisha kwamba unafanya kile ambacho unacho kwenye akili yako.
Rafiki yangu kama unataka wazo lako lifahamike dunia nzima, basi huna budi kuhakikisha kwamba unaanza kulifanyia kazi sasa hivi ili siku ya siku tuweze kuliona likiwa katika kitu ambacho kinagusika au kitu ambacho kinafanya kazi.
Acha kujifungia huko na wazo lako. Amka sasa hivi ili uende kulifanyia kazi wazo lako sasa hivi.
Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA