Hivi Ndivyo Wewe Unapaswa Kufikiri


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo rafiki yangu. Nina hakika leo ni siku ya kipekee sana maishani mwako.

Hongera sana kwa siku hii.

Leo ngoja tuzungumze namna ya kufikiri ambayo unapaswa kuwa nayo.

Bila shaka umewahi kusikia, kila mtu yuko alivyo kwa sababu ya jinsi anavyofikiri. Ikimaanisha kwamba kama mtu anafikiri uzuri, uzuri unakuja kwake. Kama anafikiri ubaya, ubaya nao unamfuata.

Kumbe kwa namna hii, basi lazima tuwe na namna nzuri ya kufikiri itakayotuwezesha sisi tufike tunapotaka. Swali la kwanza la kujiuliza ni je, unafikiri nini sasa hivi?
Je, unafikiri uzuri au ubaya.
Unafikiri utajiri au umasikini?
Unafikiri ukuu au udogo?
Jiulize kwanza maswali haya.

Namna nzuri ya kufikiri ni kuchagua kitu kimoja. Kukiwekea malengo na kukiweka katika akili yako.

Hakikisha kwamba muda woote unafikiri juu ya lengo lako au ndoto yako hii. Kila hatua upigayo. Kila mahali uendapo, fikiria juu ya malengo yako. Fikiria jinsi ya kuyakamilisha. Fikiria jinsi ya kuongeza kitu cha ziada kwenye malengo yako. Fikiria unavyoweza kusonga mbele.

Hii ndio namna nzuri ta kufikiria kwenye maisha yako. Kama kitu hakipo kwenye malengo yako basi hamna haja ya kupoteza muda ukikifanya.

Asante sana,


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X