Huu Ndio Upande Unaopaswa Kuuchagua Siku Zote


Katika historia ya dunia tunasoma kwamba mwaka 1884 kulikuwa na mkutano wa Berlin. Katika mkutano huu nchi za Ulaya zilikuwa zikipambana ili kuhakikisha kwamba zinaligawa bara la Afrika.

Mmoja wa watu waliokuwepo kwenye mkutano huo ni Marekani. Lakini Marekani hakuwa mmoja wa watu waliokuwa wanapigana ili kupata sehemu Afrika, bali Marekani alikaa kama msikilizaji.

Rafiki yangu, sijaandika kidokezo hiki bure tu ndani ya siku hii ya leo.
Na wewe kuna nyakati watu wataongea. Watu watatengeneza makundi. Lakini wewe kama wewe, unahitaji kuamua upande sahihi wa kuwepo kulingana na malengo yako.

SOMA ZAIDI; Jinsi Ya Kuepukana Na Kauli Hizi Tatu Za Kukatisha Tamaa

Kama utaona pande hizi zote hazikufai, basi kaa tu usikilize. Sikiliza pande zote zikiongea, sikiliza pande zote zikiumana na mwisho wa siku fanya kile ambacho ni sahihi.

Kwa hiyo upande mzuri wa wewe kuwepo siku zote ni upande sahihi.

ONYO: Jambo hili halipaswi kuwa chanzo cha wewe kutochukua hatua. Hakikisha kwamba pale unapopaswa kuchukua hatua unachukua hatua, na pale ambapo hapaeleweki basi unaachana na huko.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X