Huu Ni Ugonjwa Ambao Unapaswa Kuuugua


 Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele. Karibu sana katika makala haya ya siku hii ya leo ambapo tunaenda kujifunza ugonjwa ambao unapaswa kuugua maishani mwako.

Kwanza igundulike kwamba kuna magonjwa mengi sana ambayo watu wanaugua hapa duniani. Magonjwa mengine yanatibika na mengine hata hayatibiki. Lakini kuna ugonjwa mmoja muhimu saaana ambao unapaswa kuugua maisha yako yote. Yaani ugonjwa huu haupaswi kutibiwa. Na ugonjwa huu sio mwingine bali ni ugonjwa wa kufanikiwa.

Kila siku unapaswa kuwa na ugonjwa huu. Kila siku unapaswa kuwa unapiga hatua kuelekea katika hatua mpya za kutafuta mafanikio bila kuchoka.

Angalia Video hii; Tabia Tatu Unazopaswa Kuwa Nazo Kuelekea Mafanikio

Huu ni ugonjwa ambao haupaswi kuukosa kuugua. Tofauti na magonjwa mengine ambayo watu wanaugua, ugonjwa huu haujawahi  kuua mtu. Ila ni ugonjwa ambao utakufanya  upige hatua na kukuwezesha kufikia kwenye kilele cha mafanikio. ugua ugonnjwa huu bora ili uweze kufika kule ambapo wewe unataka kwenda.
Asante sana rafiki yangu, imani yangu kwamba utaugua ugonjwa huu kuanzia leo ili hatimaye tukutane kwenye kilele cha mafanikio.

Asante sana

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X