Je, Dunia Ya Sasa Ni Kijiji Au Mabara Yameongezeka?


“Dunia ya sasa hivi ni kama kijiji” huu ni usemi ambao unapedwa kutumiwa na watu wengi sana.

Watu wanatumia usemi huu wakimaanisha kwamba sasa unaweza kuwasiliana na mtu yeyote sehemu yoyote duniani na muda wowote bila shida kubwa sana kama ilivyokuwa zamani.

Tukirudi miaka ya nyuma kidogo, mpaka kwenye karne ya 15, ilichukua miezi na miezi mtu kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine ili kuwasiliana na ndugu zake.

 Ilichukua miezi na miezi mtu kutoka eneo moja mpaka jingine ili kufanya mabadilishano ya kibiashara (barter trade).

Na hapo sasa sijakurudisha kwenye enzi zileee za biashara iliyokuwa ikifanyika kuvuka jangwa la sahara maarufu kama TRANS SAHARAN TRADE.

Kumbe tukilinganisha na zama zile basi naomba niseme kwamba kweli suala zima la biashara limerahisishwa sana, sana, sana.

Lakini swali langu ni je, ni kweli DUNIA IMEKUWA KIJIJI AU MABARA YAMEONGEZEKA?
Ni kweli dunia imesogea karibu kama tunavyofikira au imezidi kusogea mbali?

Ebu na wewe tafakari hili hapa.

Tupo kwenye zama ambapo asilimia kubwa ya watu wana simu. Na ambaye hana sasa hivi basi yupo kwenye mpango wa kuwa nayo. Na tena simu ambayo mtu anapenda kuwa nayo sasa hivi ni hizi hapa zinaitwa simu janja, maarufu kama SMARTPHONE.

Je, ni kweli simu hizi zimetuunganisha na kuifanya dunia kijiji au zimetutenganisha zaidi?

Sio ajabu katika zama hizi kusikia kwamba wazazi wanapenda smartphone zaidi ya watoto. Wala sio ajabu kusikia kwamba watu wanashinda mitandaoni kuliko wanavyoshinda kwenye kujenga mahusiano yao na kazi?

Swali, NI KWELI DUNIA INAZIDI KUWA KIJIJI AU MABARA YANAZIDI KUONGEZEKA?

Imefikia hatua watu wanatengeneza clips zinazoonesha watoto mbali mbali ambao wamefikia hatua ya kutaka kuwa SMARTPHONE ili nao wapendwe na wazazi wao!!!
Uh, inashangaza lakini huu ndio uhalisia.

Katika hali ya kawaida marafiki mkikutana sehemu, tunategemea kwamba mkae mpige stori, mbadilishane mawazo, na kupeana za huku na kule.

Lakini sasa mambo ni kinyume, marafiki wakikutana wakanunua soda, basi kila mtu anakuwa bize na simu yake. Kwa nini?
Naomba kuuliza ni kweli DUNIA IMEKUWA KIJIJI AU MABARA YAMEONGEZEKA?

Kibaya zaidi ni kwenye mikutano, tena mikutano ya inayohitaji maamuzi ya watu waliotulia.

Unakuta watu wanaangalia status za wasapu na facebook badala ya kujadili maamuzi ya msingi yenye manufaa.

Wanafunzi vyuoni hawasomi tena darasani, yaani ni mwendo wa kuchati hata wanapotakiwa kumsikiliza mwalimu darasani.

Ukiuliza kisingizio kikubwa wanasema tunataka kuwa updated.
Swali langu ni je, DUNIA IMEKUWA KIJIJI AU MABARA YAMEONGEZEKA?

Kuna nyakati huwa zinanishangaza, tena huwa nashangaa kweli.

Mtu anaenda kusali kanisani na huku ametegesha simu yake ikiita apokee……

mtu anakula anachati….

Wakati wa kulala mtu ameweka simu pembeni ili akitumiwa ujumbe aujibu.

Swali langu, je ni kweli DUNIA IMEKUWA KIJIJI AU MABARA YAMEONGEZEKA???

Namalizia hivyo rafiki yangu,
Naitwa
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

kabla sijaondoka kabisa nakuachia kifurushi hiki cha mwezi,

Vitabu vyangu hivi hapa sasa vitapatikana kwa punguzo kwa siku hizi tatu.

hii ni ya kwako tu

Ona hapa,

TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA- tsh. *7,000/-* badala ya
~10,000/-~

KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI tsh. *6,000* badala ya ~10,000/-~

NYUMA YA USHINDI tsh. 3,000/- badala ya ~5,000/-~

MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA tsh, 3,000 badala ya  ~5,000/-~

Humu utapata kujifunza zaidi na zaidi na kufanya maisha yako kuwa bora sana,

vitabu hivi ni soft copy na vinatumwa kwa email. Lipia kupitia 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA. baada ya hapo nitumie email yako kwenye namba hiyo.

utapokea kitabu muda mfupi baada tu kutuma pesa.

karibuni sana upate kifurushi hiki cha mwezi juu wa sita pekee👆🏾👆🏾👆🏾


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X