Nani ametengeneza kanuni hii? Haifanyi kazi!!!


Nakumbuka shule ya msingi kuna maswali ambayo usingeweza kuyafanya bila ya kuwa na kanuni. Kwa hiyo ulipaswa kumeza kanuni husika ili uweze kufanya swali fulani kwa ufanisi.

Kwa hiyo ulikiwa wajibu wa kilaw mwanafunzi kuhakikisha kanuni zilizo katika mtaala anazijua na kuzifuata. Kama ni kanuni ya mduara, basi kila mwanafunzi alipaswa kuijua haswaaa, na kuitumia vizuri kwenye swali ili apate matokeo anayotegemea.
Ukikosea kanuni unakosa swali.

Soma Zaidi: Hii Ni Fursa Ambayo Hupaswi Kuipuuza
Maisha pia yana kanuni. Yaani rahisi kiasi hicho. Ukizijua kanuni na kuzifuata, utafurahi sana. Ukivunja kanuni utavunjika mwenyewe.

Na kanuni za maisha ni rahisi sana,

Fanya mazoezi kila siku kwa dak 20 na zaidi.

Weka malengo ya maisha na yafanyie kazi.

Usile vyakula vya aina fulani.

Yaani ni rahisi sana. Lakini watu wanazipuuzia kiasi cha kutosha.

Mbali na kuzipuuzia wanakuja na kanuni zao wenyewe mpya ambazo kabisa hazifanyi kazi.

Mtu anakuja na kanuni ya kuangalia Tv masaa zaidi ya kumi. Na kweli hii ni kanuni mpya.

Mtu anajua wazi kwamba anapaswa kufanya mazoezi kila siku. Yeye anakuja na kanuni mpya ya kufanya mazoezi ya kufa na kupona mara moja baada ya miezi sita.

Yaani hii haihutaji mtaalamu kuonesha kwamba kanuni yako si sahihi.

Wewe mwenyewe unaweza kuangalia, kati ya mtu anayefanya mzoezi kila siku kwa dakika kadhaa na yule anayefanya mazoezi mara moja kwa mwaka ni yupi yupo sahihi?

Unadhani malimbikizo yote hayo unaweza kuyaondoa kwa siku moja.

Kumbe kupuuzia vitu vidogo ni rahisi sana.  Kwa hiyo badala ya kupuuzia kanuni hizi ndogo ndogo tunapaswa kuzijua na kuzifuata.

Badala ya kusoma kitabu kizima kwa siku moja kwa fujo, ebu tujenge utaratibu wa kusoma kurasa kadhaa kila siku.

Badala ya kufanya mazoezi mara moja kwa mwaka kwa fujo. Ebu tufanye kila siku.

Badala ya kuweka akiba mara moja kwa fujo, ebu tujenge utaratibu wa kufanya hivyo kila mara.

Kwa kufanya hivi tutakuwa tumeziishi kanuni. Badala ya kuzivunja.

Asante sana rafiki yangu,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blospot.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X